Tuesday, October 18, 2011

JOHN MWAKILEMBE AFARIKI DUNIA BAADA YA KUUMWA NA NYUKI; WENGINE WAWILI WAJERUHIWA...

Mtu Mmoja jijini Mbeya amefariki dunia baada ya kuumwa na Nyuki.

Akithibitisha kutokea tukio hilo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ANECLATUS MALINDISA amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo John Mwakilembe mwenye umri wa miaka 50 mkazi wa Isanga alipatwa na mkasa wa kung’atwa na nyuki Oktoba 16, mwaka huu majira ya saa saba mchana huku wengine wawili kujeruhiwa.

Miongoni mwa waliojeruhiwa na nyuki hao ni pamoja na Mboka Masapa na Meblon Mofat.

mara baada ya watu hao kujeruhiwa wamekimbizwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya ambako wanaendelea kupatiwa matibabu

No comments:

Post a Comment