Seneta John MacCain wa Marekani amemtahadharisha Rais Barak Obama wa nchi hiyo kuhusu athari za kutuma wanajeshi wa nchi hiyo nchini Uganda na huko katikati mwa Afrika.
Mac Caina amesema, kuna wasiwasi kwamba hatua hiyo ya Marekani inaweza kuzusha vita vipya.
John MacCain ameongeza kuwa kwa bahati mbaya serikali ya Washington kwa mara nyingine tena imeamua kuchuka hatua hiyo ya kutuma wanajeshi huko Uganda na katikati mwa Afrika bila ya kushauriana na Congress.
Serikali ya Marekani Ijumaa iliyopita ilitangaza kuwa itatuma washauri wa kijeshi mia moja huko Uganda ili kusaidia kupambana na waasi wa eneo la katikati mwa Afrika.
Kundi la waasi wa jeshi la Kikristo wa kaskazini mwa Uganda wanaoongozwa na Joseph Kony linaendesha mapigano huko katikati mwa Afrika kwa miaka kadhaa sasa.S
No comments:
Post a Comment