Taarifa ya jeshi la polisi mkoa wa mbeya kwa vyombo vya habari
“press release” tarehe 02. 02.2013.
Wilaya ya mbarali - muendelezo wa taarifa ya ajali ya
gari kupinduka na
Kusababisha
vifo na majeruhi.
Mnamo tarehe
01/02/2013 majira ya saa 07:15hrs huko kapunga chimala wilaya ya mbarali mkoa
wa mbeya.
Gari namba t.398
bse scania tipper 114 model mali
ya mwekezaji aitwaye kapunga rice project likiendeshwa na dereva aitwaye baraka
s/o mollel , miaka 29,mmasai na mkazi wa matebete likiwa limebeba vibarua wa
kupanda mpunga kutoka kijiji cha mapogoro kwenda katika shamba la mwekezaji .
Gari hilo likiwa ndani ya shamba hilo liliacha njia na kupinduka kisha
kusababisha vifo vya watu wanne [4] ambao ni 1. Samweli s/o mapugilo, mbena, 30yrs
na mkazi wa ilembula 2. Bon s/o mfupa, mnyakyusa, 27 yrs mkazi wa
mapogolo na 3. Edgar s/o mwakipesile, miaka 35, kyusa, mkulima
mkazi wa nonde mbeya na 4. Tazama s/o kazembe,miaka 34,msafwa,mkulima
mkazi wa mswiwsi ambaye amefariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu
hospitali ya rufaa mbeya. Aidha katika
ajali hiyo watu 130 walijeruhiwa kati yao wanaume 89 na wanawake 41. Majeruhi
74 kati yao wanaume 49 na wanawake 25 walipelekwa
hospitali ya misheni chimala kwa ajili ya matibabu ambapo majeruhi 44 walipatiwa
matibabu na kuruhusiwa na majeruhi 30 kati yao wanawake 14 na
wanaume 16 wamelazwa hospitalini hapo wakiendelea kupatiwa matibabu. Aidha
majeruhi wengine 56 waliopelekwa hospitali ya rufaa mbeya 22 walipatiwa
matibabu na kuruhusiwa na majeruhi 34 wamelazwa hospitali hapo kwa
matibabu zaidi kati yao
wanawake 8 na wanaume 26 .
Mpaka sasa jumla ya majeruhi 64 bado
wamelazwa katika hospitali za rufaa mbeya na chimala misheni hali zao
zinaendelea vizuri na majeruhi 66 walipatiwa matibabu katika hospitali
hizo na kuruhusiwa.
Chanzo cha
ajali ni mwendo kasi uliosababishwa na vibarua waliokuwa ndani
ya gari hilo
kumshangilia dereva na gari lilipofika
kwenye kona lilimshinda kukata kona na kupinduka. Dereva alikimbia mara baada ya tukio. Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna
msaidizi wa polisi diwani athumani anatoa wito kwa madereva kuwa makini
wanapokuwa barabarani kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha
ajali zinazoweza kuepukika.
Aidha anatoa wito
kwa mtu/watu wenye taarifa mahali alipo dereva azitoe ili akamatwe vinginevyo
ajisalimishe mara moja. Pia anaendelea kuwaasa wananchi kuacha tabia ya
kuwashabikia madereva wanaoendesha vyombo vya moto kwa mwendo kasi kwani
inaweza kuhatarisha maisha na mali
zao.
Signed by,
[diwani athumani – acp]
Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya.
No comments:
Post a Comment