Na Danson
Kaijage wa Habarika Blog
JESHI la
polisi nchini limeendelea kuandamwa na mzimu wa mauaji ya raia wasiokuwa na hatiai
baada askari polisi aliyefahamika kwa jina moja la (Manase) kutuhumiwa kumpiga mwananchi
na kusababisha kifo.
Maiti ya Rashid Juma aliyepigwa risasi na askari polisi ikiwa imelazwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Wilaya Bukombe.(Picha na Danson Kaijage) |
Hali hiyo imejitokeza leo Novemba 24 katika kituo cha
polisi cha Ushirimbo Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita, ambapo askari polisi
amempiga risasi na kumuua kijana ambaye amefahamika kwa jina la Rashid Juma (23).
Tukio la
polisi kumuua kijana huyo limesababisha tafrani kubwa baina ya polisi na wananchi
wenye hasira kali ambao wamevamia kituo hicho kwa lengo la kulipiza kisasi kwa
kuchoma moto kituo hicho na kutaka askari aliyehusika na mauaji ya kijana huyo
naye auwawe.
Hata hivyo askari
walilazimika kutumia nguvu nyingi kwa kurusha mabomu ya machozi, risasi za moto
na risasi baridi kwa ajili ya kuwatawanya wananchi hao ambao walikuwa wakirusha
mawe kwa lengo la kuwajeruhi askari hao na kuharibu mali za kituo hicho.
Tukio hilo
limetokana na askari ambao walikwenda kumkamata mtu ambaye anadaiwa kuwa ni
jambazi na aliyesadikiwa kuwa alikuwa amejificha katika nyumba ambayo ipo
katika mtaa wa Kilimahewa mjini Ushirombo,
ambapo askari
hao walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo na kumweka ndani ya gari.
Baadhi ya
wananchi wameonekana kulizingira gari hilo huku wakitaka mtuhumiwa huyo atolewe
kwenye gari ili auwawe.
Katika kukabiliana
na hali hiyo askari wamelazimika kufyatua risasi juu kwa lengo la kuwatawanya
wananchi na ndipo askari mmoja alipomlenga kijana huyo risasi ya kiunoni na
kijana huyo kupoteza maisha hapo hapo.
Baada ya
kuzuka kwa ghasia hizo za wananchi kutaka kuchoma kituo, mbunge wa Bukombe,
Peofesa Kulikoyela Kahigi(Chadema) akiwa ameambatana na Diwani wa kata ya
Igulwa, Soud Ntanyagalla (Chadema)walituliza ghasia hizo kwa kuwasii ndugu wa
marehemu paomaja na mama yake mzazi Justina Fransis kwa madai kuwa
watashughulikia suala hilo.
Mbunge pamoja
na Diwani walimtaka mkuu wa Polisi Wilaya kuambatana naye hadi kwenye hospitali
ya Wilaya ili kujilidhisha kama kijana huyo ambaye alipigwa risasi kama
amefariki ama yuko mahututi.
Viongozi hao
walitaka kufika hospitalini hapo kutokana na Mkuu wa Polisi kudai kuwa kijana
huyo yupo hai na anaendelea na matibabu.
Hata hivyo
baada mbunge na diwani kufika katika hospitali ya Wilaya ya Bukombe, Mganga Mkuu
wa Wilaya Dk.Archard Rwezahura alithibitisha kuwa kijana huyo ambaye alipigwa
risasi na polisi alifia mikononi mwa polisi na wala siyo hospitalini kama
ilivyokuwa ikidaiwa na jeshi la polisi.
Kwa upande
wake Mkuu wa Polisi Mkoa wa Geita (RPC) Lenard Paul alipoulizwa juu ya tukio
hilo alikiri kupata taarifa ya kijana huyo kupigwa risasi na kufa,akaahaidi kuwa
hatua za kisheria zitachukuliwa kwa
askari aliyehusika.
Kwa upande
wa viongozi kwa maana ya Mbunge na Diwani wamewaahidi wananchi kuwa watashughulikia
suala hilo na wamelitaka jeshi la polisi lichukue hatua za kisheria kwa askari
huyo.
No comments:
Post a Comment