Tuesday, October 18, 2011

MBEYA: WATU WA3 WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI MLIMANYOKA...

WATU wapatao watatu wamepoteza maisha katika ajali ya gari Mlima Nyoka nje kidogo ya Jiji la Mbeya.

Mashuhuhuda wa Ajali hiyo wamesema ajali imetokea majira ya saa 3:45 usiku wa Oktoba 18 ikihusisha magari mawili Toyota Hiace na Suzuki Escudo.

Wengine waliokuwemo kwenye magari hayo wamejeruhiwa.

Wakati huo huo mtu asiyefahamika amegongwa na gari maeneo ya Mwanjelwa Jijini Mbeya majira ya saa 4:00 usiku na kujeruhiwa.

Gari lililomgonga mtembea kwa miguu huyo limetoweka kusikojulikana

No comments:

Post a Comment