Saturday, January 26, 2013

ORODHA NA PICHA ZA MAGARI YENYE SURA MBAYA DUNIANI

 
Black Falcon,ambalo limeundwa na Kampuni ya DARTZ Motorz Company,ya Uchina

 
Sehemu ya Tangazo la Gari hilo linalotarajiwa kuanza kuuzwa katika soko la magari la Mashariki ya Kati na Arabuni mapema mwaka huu

 
Gari hilo Black Falcon kama linavyoonekana kwa ndani; Limetengenezwa kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya NYOKA inayosherehekewa nchini China

GARI BAYA ZAIDI KUWAHI KUTENGENEZWA DUNIANI...Ona hapo chini...






PICHA JUU: TOYOTA BB miongoni mwa magari yanayotajwa kuwa mabaya zaidi duniani

 
Miongoni mwa mengine pia limo Aston Martin Lagonda hilo hapo juu.



600-Aurora huenda likavunja rekodi,ambalo limeelezwa kufanana na mnyama Faru anaemkimbiza adui yake! baadhi ya Watoto wakiliona hili huanza kulia akiwemo mtoto wa Martin Jusper wa Uingereza anaelimiliki

Maelezo ya hili yamejitosheleza katika picha AMC PACER ambalo liliundwa mwaka 1975.Ni baya lakini limeelezwa kuwa miongoni mwa magari yenye spidi kubwa enzi hizo.

Orodha bado ni ndefu; Pichani ni CHEVROLET CORVAIR ambalo likisahaulika 'haki haijatendeka!

Kampuni ya Magari ya FORD ni miongoni mwa makampuni maarufu ya magari duniani lakini hapa 'designing' iliwashinda! Hilo ni FORD EDSEL  liliundwa miaka 50 iliyopita.

Chevrolet hivi leo ni gari inayopendwa na kuhusudiwa na wapenzi wa magari duniani lakini designing hii duh! Hiyo ni Chevy Chevette
 iliyoundwa miaka kama 60 iliyopita lakini baada ya kutembea 40,000 Injini yake ikasambaratika kutokana na 'kuchemsha'

NAWATAKIA WEEKEND NJEMA...


   

1 comment: