Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) inapenda kuueleza umma kuwa taarifa
zinazotolewa na kikundi kinachoongozwa na Chaurembo Palasa za kuitisha mkutano
wa kuhakiki wanachama ni potofu kwani wanachama wa TPBC ni Kamisheni za mikoa
na haina wanachama mmoja mmoja katika ngazi ya taifa.
Katiba ya TPBC iliyotoka
mwaka 2001 imetamka wazi kuwa wanachama wa TPBC ni Kamisheni za Mikoa.
Hakuna
mwanachama wa TPBC anayeitwa Chaurembo Palasa. Kadi ya uanachana anayoitembeza kwenye
mitandao ni ya zamani kabla ya katiba ya TPBC kubadilika na kufuta uanachama
wake.
Yeye
mwenyewe alishiriki kama mwanachama wa kutoa maamuzi ya kikao kilichofuta
uanachama wake kwani ilionekana kuwa mabondia wanatumika kuleta fujo kama
anavyotumika yeye hivi sasa.
Bwana Chaurembo Palasa anakaribishwa kuleta maoni yake kuhusu namna ya
kuboresha shughuli za TPBC kama alivyojitokeza na kwenda kulipa ada
(japokuwa waliingilia jambo lisilowahusu).
Yeye na kikundi chake
wanaendelea kuchukua marejesho (refund) ya pesa hizo kila mwezi kutoka
kwa Mweka Hazina wa TPBC bwana Boniface Wambura.
Chaurembo
na kikundi chake kinachoongozwa na kiongozi mmoja wa chama cha ngumi za
kulipwa na ambaye ameamua kuleta fujo ili kufifisha juhudi za TPBC za
kuleta maendeleo ya ngumi nchini wanataka kuturudisha kwenye migogoro
isiyoisha ya miaka ya 80 na 90 ambayo ilitawala tasnia ya ngumi
Tanzania.
Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) imepanga kuanza
kufanya uchaguzi tarehe 31 March 2013 kuchagua viongozi wapya watakaoiongoza
Kamisheni hiyo.
Uchaguzi huo utaanzia ngazi za mikoa kwa kuchagua Makamishna
wa mikoa pamoja na Kamati za Utendaji. Kilele cha uchaguzi huo kitakuwa ngazi
ya taifa ambako viongozi wakuu kuanzia Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Mweka
Hazina na wajumbe wa Kamati ya Utendaji watachaguliwa. Nafasi ya Urais ni ya
heshima ambapo atateuliwa na Kamati ya Utendaji pamoja ya ile ya Katibu
Mtendaji ambayo ni ya kuajiriwa!
Rais wa sasa Onesmo Alfred McBride Ngowi hatatetea tena
kiti chake baada ya kuiongoza TPBC kwa takribani miaka kumi (10)!
Ngowi amewataka watanzania walio na uwezo pamoja na nia ya
kuiongoza Kamisheni hiyo wajitokeze ili waweze kugombea nafasi za uongozi.
Ngumi za Kulipwa zimekuwa ni ajira na ni vyema tukapata viongozi wazuri wa
kuiongoza TPBC ili waweze kutoa nafasi za ajira kwa vijana!
Viongozi wa sasa wa TPBC ni:
Onesmo A.M. Ngowi -
Rais
Madaraka Nyerere - Makamu
wa Rais
Nemes Kavishe -
Katibu Mkuu
Nicholaus Mallya -
Naibu Katibu Mkuu
Boniface Wambura -
Mweka Hazina/ Mwenyekiti wa Viwango
ZIADA:
BIBLIOGRAFIA YA CHAUREMBO PALASA HII HAPA
Chaurembo Palasa | ||||
---|---|---|---|---|
Global ID | 53873 | |||
sex | male | |||
division | light welterweight | |||
stance | orthodox | |||
alias | Firestone | |||
country | Tanzania | |||
residence | Dar-Es-Salaam, Tanzania | |||
birth place | Dar-Es-Salaam, Tanzania | |||
rounds boxed 249 KO% 31.58 | ||||
No comments:
Post a Comment