Diwani wa Kata ya Uwemba Wilayani Njombe Bw Edward Mwalongo Amewataka Wananchi Kushirikiana na Serikali Pamoja na Mashirika Mbalimbali Kusaidia Watoto Yatima na Wanaoishi Katika Mazingira Hatarishi Kwa Kutoa Misaada Itakayowasaidia Watoto Hao Kumudu Changamoto Zinazowakabili
Akikabidhi Misaada Kwa Watoto Yatima 28 Katika Kata ya Uwemba,Bw Mwalongo Amesema Pamoja na Jitihada Zinazofanywa na Mashirika Yasio ya Kiserikali Katika Kusaidia Watoto Hao Lakini Bado Misaada Hiyo Imekuwa Haitoshelezi Mahitaji ya Watoto Hao Kutokana na Uwezo Mdogo Unaokabili Mashirika Hayo
Aidha Diwani Huyo Ameahidi Kutoa Shilingi Milioni Tano Kwa Ajili Ya Kukisaidia Kikundi Hicho Katika Kuendeleza Shughuli Za Kimaendeleo Ikiwa Ni Pamoja Na Kuwasomesha Watoto Wawili Wakiume Na Wakike Kwa Kuwa Lipia Ada Ya Shule Kuanzia Kitado Cha Kwanza Hadi Cha Nne Katika Shule Ya Sekondari Ya Hagafilo
Katika Hatua Nyingine Diwani Mwalongo Amevita Vikundi Vya Kijasiliamali Na Taasisi Nyingine Kufanya Kazi Kwa Kushirikiana Na Idara ZaMaendeleo Ya Jamii Zilizoko Katika Maeneo Yao Ili Viweze Kufanya Shughuli Zao Kwa Kufuata Katiba Na kisheriaKatika Risala Yao Iliyosomwa Mbele Ya Mgeni Rasmi Na Mkurugenzi Wa Vikundi Vya SILC Wilayani Njombe Bwana Emmanuel Kimbe Amesema Lengo La Kuanzisha Vikundi Hivyo Ni Kujikwamua Kiuchumi Na Kuomdokana Na Umasikini Kwa Wajasiliamali Wadogo Wadogo Kwa Kuweka Na Kukopeshana Mitaji Midogo
Hata Hivyo Mkurugenzi Huyo Ameongeza Kuwa Kutokana Na Kukua Kwa Na Kuimarika Kwa Vikundi Hivyo Wameamu Kuyasaidia Baadhi Ya Makundi Katika Jamii Kama Watoto Yatima Na Wale Wanaoishi Katika Magumu Pamoja Watu Wasio Na Uwezo.
No comments:
Post a Comment