Tuesday, October 11, 2011

MBUNGE KILUFI WA MBARALI: APANDISHWA KIZIMBANI

MBUNGE WA MBARALI MODESTI DICKSONI KILUFI (51) JANA AMEFIKISHWA KATIKA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI JIJINI MBEYA KUJIBU SHTAKA LINALOMKABILI LA KUMDHALILISHA NA KUMTISHIA KIFO JORDAN MASWEVE

AKISOMA SHAURI HILO MAHAKAMANI HAPO WAKILI WA SERIKALI GRIFIN MWAKAPEJE MBELE YA HAKIMU MKAZI MICHAEL MTEITE AMESEMA KATIKA MAENEO YA UBARUKU MBARALI MBUNGE HUYO ALITISHIA KUMWUA JORDAN MASWEVE AMBAPO NI KOSA KINYUME NA KIFUNGU CHA SHERIA NAMBA 89 IBARA YA (2) "A" KILICHOFANYIWA MAREKEBISHO MWAKA 2002

NAO UPANDE WA UTETEZI MAHAKAMANI HAPO ULIOMBA DHAMANA AMBAYO HATA HIVYO MAHAKAMA HAIKUTOA PAPO KWA KUSEMA WAKATI UAMUZI WA KUTOA DHAMANA UNAFIKIRIWA MTUHUMIWA ATAKWENDA RUMANDE HADI TAREHE 24/10/2011 KESI HIYO ITAKAPOTAJWA TENA

No comments:

Post a Comment