Na:Francis Godwin
Watu
wasiofahamika wameingia nyumbani kwa mkuu wa mkoa wa
Njombe [RC]
Kaptain Mstaafu Asseri Msangi usiku wa kuamkia
leo na kuiba
vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni
moja.
Akizungumza
na mwandishi wa mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com mkoani Njombe
Gabriel Kilamlya Kaptaini Msangi alisema tukio hilo lilitokea usiku wa manane
wakati
amelala, na
alivitaja vitu vilivyoibiwa kuwa ni pamoja na kidadavuo
mpakato
[laptop] yenye thamani ya shilingi laki saba na nusu pamoja
na simu tatu
za vijana wake zenye thamani ya shilingi ya laki nne na
nusu.
Hata hivyo
Kaptaini Msangi alisema tukio hilo limemsikitisha sana
hasa
ikizingatiwa kwamba nyumba yake inalindwa na askari wa jeshi
la polisi
wenye bunduki zenye risasi za kutosha.
"Nimeishi
miaka mingi kwenye nyumba bila ulinzi wowote nilipo
kuwa mkuu wa
wilaya [DC] sijawahi kuibiwa lakini leo hii mkuu wa
mkoa nina
walinzi lakini nimeibiwa, mpaka hapa naona haina haja ya
kuwa na
walinzi"alisema Msangi.
Aidha Msangi
alisema anawatilia shaka askari polisi waliokuwa zamu
huku kuwa
wanahusika na tukio hilo.
Mkuu huyo wa
mkoa aliongeza kuwa wakati mwingine walinzi hao
huwa
wanatoroka lindo na kwenda kunywa pombe.
Kufuatia
tukio hilo jeshi la polisi mkoani Njombe linawashikilia
askari
wawili wa jeshi hilo waliokuwa lindo kwa mkuu wa mkoa
usiku huo wa
tukio kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Akizungumza
na mtandao huu kamanda wa jeshi la polisi mkoani
Njombe
Fulgency Ngonyani aliwataja askari hao kuwa ni pamoja na
askari
mwenye namba G. 5414 PC Ombeni na askari mwenye
namba G.
5455 PC Mohamed ambao wakati tukio hilo likitokea ndio
waliokuwa
zamu ya kulinda kwa mkuu huyo wa mkoa.
"Tunawashikilia
askari hawa kwa kuwa ndio walikuwa lindo, lakini
hata hivyo
tumefanya uchunguzi wa awali hatujaona sehemu yoyote
iliyobomolewa
yawezekana watu walifanya tukio hilo la wizi
walitumia
funguo bandia" alisema Kamanda Ngonyani.
Akizungumzia
hataua ya askari wa jeshi hilo kuwa na tabia ya
kuacha lindo
na kwenda kunywa pombe, Kamanda Ngonyani alisema
hana taarifa
hizo lakini aliahidi kulifanyia kazi, ambapo amemwagiza
mkuu wa
upepelelezi kufanya uchunguzi juu ya jambo hilo.
No comments:
Post a Comment