Tuesday, October 11, 2011
WAGONGA NONDO 26 WADABULIWA NA JESHI LA POLISI MBEYA
Jeshi laPolisi Mkoani Mbeya limewatia nguvuni watu 26 wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya kutumia silaha kama vile, Nondo na Mapanga.
Akithibitisha kukamatwa kwa watu hao Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Advoketi Nyombi amesema, watu hao wamekamatwa katika makundi matatu ambapo Kundi la Kwanza lina watuhumiwa wanne, kundi la Pili lina watuhumiwa saba,na kundi la Tatu lina watu Kumi na watano ambapo mbali na watuhumiwa hao kushikiliwa pia wanashikiliwa na silaha kama Nondo na Mapanga
Amesema,miongoni mwa waliokamatwa na kukiri kuhusika katika Mauaji ya RICHARD SHITAMBALA aliyeuwawa eneo la Uyole ni pamoja na Herodi Lukas (28), mkazi wa Ilemi,Mussa Iddi (30), mkazi wa Ilemi,Fadhil Luvanda (25) Mkazi wa Makunguru na Devid Jimmy (19) Mkazi wa Mwanjelwa.
Ameongeza kuwa watuhumiwa wengine wamekiri kuhusika na mauaji ya Askari Polisi ambao amewataja kuwa ni EDISENI ULENDO (24) mkazi wa Mwanjelwa,Rashid Mwakyandwe (25) mkazi wa Itiji,Erasto Elias (23) mkazi wa Mabatini Mussa Lukose (28) Mkazi wa Ilolo Sinde, Amos Mziho (26) Mkazi wa Mbozi, Sifa Njowela (25) Mkazi wa Vyawa Mbozi Frank Kitonga Njowela (29) Mkazi wa Itende
Ameongeza kuwa watuhumiwa wengine Kumi na Tano bado wanafanyiwa uchunguzi ili kubaini endapo wanahusika na vitendo vya upigaji nondo na kwamba mara baada ya uchunguzi kukamilika hatua zaidi za sheria zitachukua mkondo wake.
Amewataka wananchi kuendelea na Kazi zao bila wasiwasi kwani Jeshi La Polisi linashughulika kutokomeza vitendo vya upigaji nondo na mauaji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment