MONDULI 19/10/2011 usiku
Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu wa Zamani wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Edward Ngoyai Lowassa amesema kamwe hana mpango wa Kumhujumu Rais Jakaya Kikwete kama Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM kama inavyodaiwa na baadhi ya vybombo vya habari
Akizungumza hii leo katika mkutano wake na wanahabari jimboni Monduli Lowassa amesema baadhi ya watu wamezua uvumi kwamba yeye amekuwa akijihusisha na kundi la kisiasa ndani CCM linalotaka kumhujumu Mwenyekiti wa Chama Rais Jakaya Kikwete.
Lowassa amesema,madai hayo hayana ukweli wowote na ameyaita ya kipuuzi,kizushi na yenye malengo machafu dhidi yake.
Ameongeza kuwa, watu hao ambao amewahusianisha na baadhi ya vyombo vya habari amesema wamedai kuwa ameanza kuandaa orodha ya kile wanachodai kuwa ni makosa ya Mwenyekiti wa CCM ambayo watu hao wamedai kuwa Lowassa amepanga kuyasoma wakati wa kikao kijacho cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM.
Lowassa Amekanusha madai hayo na kusema kuwa yeye kama Mwenyekiti wa Kamati Nyeti ya bunge ya Mambo ya Nje,Ulinzi na usalama na zaidi amewahi kuwa kiongozi wa juu wa serikali kama Waziri Mkuu hawezi kufanya kitendo hicho cha kikihujumu chama na Mwenyekiti wake.
Amewataka waandishi wa habari kuandika habari zitakazoibua masuala ya uimarishwaji wa utawala bora,kuporomoka kwa thamani ya shilingi,mdororo wa uchumi,tatizo la ajira kwa vijana,kushuka kiwango cha elimu nchini na ugumu wa maisha unaowakumba wananchi badala ya kujadili maisha binafsi ya watu ambayo hayana tija kwa maendeleo ya Taifa.
No comments:
Post a Comment