Sunday, October 9, 2011

WAHADZABE,WAIRAK NA WAMBULU WANAKUMBWA NA NJAA MKOANI MANYARA!!



HUKO MKOANI MANYARA WATU WA JAMII YA KIHAZABE,WAIRAK NA WAMBULU WANAOISHI KATIKA BONDE LA YAEDA CHINI WANAKABILIWA NA NJAA KALI PAMOJA NA UPUNGUFU WA CHAKULA AMBAPO TAARIFA ZA SHIRIKA LA TAIFA LA UTANGAZAJI TBC ZINASEMA WATU HAO WANASHINDIA UBUYU

BAADHI YA WAKINA MAMA WAMEIAMBIA TBC KUWA HALI YA MAMBO KATIKA ENEO HILO SIO NZURI KWANI WANAKUMBWA NA UHABA WA MAJI,CHAKULA NA WANASEMA WANAHITAJI MSAADA.

DIWANI WA KATA YAEDA CHINI BRYSON MAGOMBE ANASEMA KWA SASA WAMEPATA CHAKULA KIDOGO AMBACHO ANASEMA KITAWASAIDIA KWA MUDA MFUPI KABLA HAWAJAHITAJI CHAKULA ZAIDI.

JAMII HIYO IMEKUWA IKITEGEMEA ZAIDI SHUGHULI ZA UWINDAJI, NA KULINA ASALI KAMA TEGEMEO LA KUWAPA CHAKULA LAKINI HALI KWA SASA SI SHWARI KWANI WANYAMA PORI WAMEPUNGUA KUTOKANA NA UKAME NA MISITU INAENDELEA KUPUKUTIKA KUTOKANA NA SHUGHULI ZA KIBINAADAMU

No comments:

Post a Comment