Saturday, October 22, 2011

OBAMA: TUMECHOKA KUKAA IRAQ KABLA YA DISEMBA TUTAKUWA U.S.A...MIAKA 9 INATUTOSHA

NEW YORK 22/10/2011 USIKU

Rais Barack Obama wa Marekani amesema kuwa vikosi vya nchi hiyo vitaondoka kikamilifu nchini Iraq ifikapo mwishoni mwa mwaka huu kama ilivyoafikiwa katika makubaliano ya usalama yaliyosainiwa kati ya pande mbili.


Obama alitangaza uamuzi huo jana Ijumaa baada ya kuwepo wasiwasi kwa miezi kadhaa kwamba huenda Marekani ikaongeza muda wa kubaki majeshi yake Iraq hata baada ya mwaka huu.


Nouri al Maliki Waziri Mkuu wa Iraq amesema kwamba baada ya karibu miaka 9 ya kuvamiwa Iraq, sasa vita vya Marekani nchini humo vitamalizika.


Mwezi Agosti uliopita Marekani ilitangaza kusitisha operesheni zake za kijeshi Iraq lakini hata hivyo ilibakiza askari wake 45,000 nchini humo kwa kisingizo cha kutoa mafunzo na ushauri kwa vikosi vya usalama vya Iraq.

No comments:

Post a Comment