Monday, October 24, 2011

EURONEWS: KAMA WAZUNGU WASINGEKUWA NA RUZUKU YA MAISHA WENGI WAO NI MASIKINI KUPINDUKIA

BRUSSELS, 24/10/2011

Imebainika kuwa watu milioni 80 wanaishi chini ya mstari wa umaskini.

Televisheni ya Euro News ya barani Ulaya imethibitisha takwimu hizo na kuongeza kuwa, kama zisingelikuwepo taasisi zinazotoa misaada kwa watu wenye shida na njaa, basi watu wengi wangelikufa kwa njaa barani humo.

Televisheni hiyo imefafanua zaidi kuhusu hali mbaya ya ukata na umaskini katika nchi za Ulaya hususan Ufaransa na kusema kwamba, kila siku kundi moja la watu wanaofanya kazi na taasisi za kutoa misaada ya kibinaadamu huenda kwenye maeneo ya kuuza matunda ili kutafuta matunda na mbogamboga zisizo na wateja na kuchambua zilizo nzima kwa ajili ya kuwapelekea watu maskini.

Taasisi hizo za kutoa misaada ya kibinaadamu barani Ulaya zinasema kuwa, idadi ya watu wanaohitajia misaada yao imeongezeka kwa asilimia mia moja jambo ambalo linaonesha kuwa idadi ya watu maskini barani humo imeongezeka maradufu.

No comments:

Post a Comment