Njombe 22/10/2011
Halmashauri ya wilaya ya njombe imetangaza kuruhusu kuendelea kwa biashara ya nguruwe kwa kufuata masharti ya wataalamu huku pia ikilegeza masharti ya karantini iliokuwa imewekwa tangu mwezi july mwaka huu
akitangaza uamuzi huo hivi leo katika kikao cha baraza la madiwani,mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya njombe bw vallence kabelege amesema hadi kulegezwa kwa masharti hayo jumla ya nguruwe 730 wamekufa kutokana na ugonjwa huo na mabanda 915 yakiwa yamepuliziwa dawa kwa ajili ya kuua virusi vya ugonjwa huo
aidha bw kabelege amewataka wafugaji kuzingatia masharti yaliowekwa na wataalamu ili kuhakikisha ugonjwa huo unatoweka kabisa huku akielezea matumani yake ya kuona mapato ya ushuru wa ukaguzi wa nyama yakiongezeka baada ya kuruhusiwa kwa biashara hiyo
No comments:
Post a Comment