Ismani, IRINGA 22/10/2011
Mbunge wa Ismani William Lukuvi ametoa msaada wa Pikipiki kwa vtuo vine vya Polisi vya Idodi,Pawaga,Migori na Ismani kwa lengo la kuvisaidia vituo hivyo kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa
Mwandishi wa Ushindi Redio Mkoani Iringa amesema kabla ya Askari Polisi hao kupewa msaada wa Pikipiki hizo walikuwa wakipata shida ya usafir ambapo mara nyingi walikuwa wakilazimika kusafiri kwa baiskeli kwenda umbali mrefu hali ambayo haiyumkini ilikuwa ikisababisha kasi ndogo ya utekelezaji wa majukumu ya jeshi hilo kwa wananchi ikiwa ni pamoja na harakati za kuwasaka wahalifu katika maeneo yao ya utekelezaji.
Msaaada huo una thamani ya shilingi za Kitanzania milioni 5 ambapo Msaidizi wa Mbunge huyo Thom Malenga amesema Lukuvi amelazimika kutoa msaada huo kutokana na kuona adha ambayo jeshi la Polisi limekuwa likipata katika Jimbo la Ismani na pia akiwa na lengo la kuimarisha ulinzi katika eneo hili la Ismani.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Evarist Mangalla amempongeza Mbunge huyo na kuwaomba wananchi na wafanyabiashara wengine wenye uwezo kuendelea kujitokeza kulisaidia jeshi la Polisi ili liweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa ukizingatia kampeni ya kuwasaka wahalifu ambayo jeshi lapolisi mkoani Humo inaiendesha.
No comments:
Post a Comment