Wakulima Mkoani Mbeya wamepongwezwa kwa kuwa na juhudi katika shughuli za kilimo amabapo imeelezwa kuwa uzalishaji umeongezeka kutoka tani laki saba hamsini elfu na themanini na saba 1980 hadi kufikia tani milioni 3.5 mwaka huu.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbass Kandoro wakati wa Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika maadhimisho yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Luanda Nzovwe
Aidha amesema kuwa wakulima laki tatu watapatiwa mbolea za ruzuku kwa ajili ya kupoandia na kukuzia ambapo mbolea ya kupandia itauzwa shilingi ishirini na tano na mbolea ya kukuzia itauzwa shilingi elfu ishirini.
Kuhusu suala la Elimu Kandoro Amewapongeza wakazi wa Mbeya kwa juhudi zao za kujenga shule za Sekondari na kuwataka waendelee na juhudi hiyo ili kuinua idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa katika shule hizo.
Akizungumzia suala la Miundombinu amesema, mkoa wa Mbeya ni miongoni mwa mikoa michache hapa nchini yenye mfumo mkubwa wa barabara za lami, ambapo hadi sasa mkoa umepiga hatua kwa kuwa na miundombinu bora ukilinganisha na miaka ya zamani, amesema serikali bado inaendelea na jitihada za kuboresha barabara na kwamba siku za usoni barabara mkoani mbeya zitaboreshwa zaidi.
No comments:
Post a Comment