Saturday, October 22, 2011

AJALI NYINGINE MBEYA LEO 22/10/2011

GARI NAMBA T 631 ABU aina ya Toyota Land cruiser limegongana ana kwa ana na gari jingine kubwa aina ya Isuzu FSR lenye plate namba STK 4220 Eneo la Uyole barabara ya Tunduma karibu na St.Agrrey Schools.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Askari wa Usalama barabarani ambaye tanzam1 imehifadhi jina lake kwa kuwa si msemaji wa Polisi amesema hakuna mtu aliyepoteza maisha katika ajali hiyo, isipokuwa dereva wa gari ndogo Landcruiser ambaye ndiye anasemekana kuwa chanzo cha ajali hiyo amejeruhiwa na kukimbizwa hospitali ya Mkoa Mbeya.

Kwa mujibu wa Askari huyo dereva wa gari ndogo alikuwa mwendo kasi na alikuwa akiyumba hovyo barabarani kabla ya kupoteza mwelekeo na kuligonga gari jingine dogo Landcruiser Mkonga juu kabla ya kuvaana ana kwa ana na Lori hilo mali ya Serikali.

Ajali hiyo imetokea muda wa saa mbili usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment