Saturday, October 22, 2011

RISASI za moto, mabomu ya machozi , silaha za kijadi pamoja na mawe vimerindima katika Kata ya Dodoma makulu

DODOMA 22/10/2011

RISASI za moto, mabomu ya machozi , silaha za kijadi pamoja na mawe vimerindima katika Kata ya Dodoma makulu kitongoji cha Njedengwa Manispaa ya Dodoma na kugeuza eneo hilo kuwa kama uwanja wa vita.

Hali hiyo imetokea baada ya Jeshi la polisi na Kikosi cha kutuliza Ghasia FFU pamoja na kampuni ya NAMAIK ambayo imekodishwa kutoka Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kubomoa nyumba za wakazi hao kuvamia eneo hilo majira ya 8 usiku na kuanza rasmi saa 11 alfajiri zoezi la kubomoa nyumba za wakazi hao zaidi ya 118 kwa ajili ya kumpisha mwekezaji ambaye anafahamika kwa jina la Sinana Enterprises.

Ushindi Redio ikiwa katika tukio ilishuhudia gari ambalo ni mali ya Mamlaka ya Ustawishaji makao Makuu (CDA), ikifanya kazi ya kuvunja nyumba hizo kwa uangalizi mkali wa jeshi la polisi.

Gari hilo ambalo lilikuwa na namba za Usajili SU 37839 aina ya HIDROMEK lilikuwa likivunja nyumba hizo ambazo zinakadiriwa kuwa ni zaidi ya 118.

Mbali na hilo Ushindi Fm imeshuhudia mabaunsa ambao walikodishwa na mwekezaji kwa ajili ya kubomoa nyumba hizo wakiwapiga ngumi na mateke baadhi ya wakazi ambao walikuwa wakipinga nyumba zao kuvunjwa.

1 comment:

  1. Huyu SINANA ENTERPRISES ANAMUIBIA MAMA MMOJA MJANE PALE DODOMA MAMA MJANE WA WATU AMBAE HANA MSAADA MMILIKI WA SHULE ILIYOKUWA INAITWA DODOMA NURU JAMANI HUYO SINANA ENTERPRISES NI JAMAA MMOJA HIVI ANAITWA MAIMU NA ANAJIFICHA KWA HIYO COVER YA SINANA ENTREPRISES NA ANATISHIA WATU MAISHA HUYU JAMAA NI TAPELI SANA

    ReplyDelete