Wednesday, June 3, 2015

Paka mwenye umri mkubwa zaidi duniani afariki dunia

Paka huyo alievunja Rekodi ya Dunia kwa kuwa na umri mkubwa zaidi wa miaka 27 akiitwa 'Tiffany Two' amekufa akiwa kwenye usingizi.

Kifo chake kimewashtusha wapenzi wa wanyama wa kufugwa nyumbani nchini Marekani ambapo kitabu cha Rekodi za dunia Guiness Book kimeweka kumbukumbu kuwa Paka huyo mwenye umri wa miaka 27 alizaliwa
Machi 13, 1988, huko  San Diego, California, Marekani.

Paka huyo alinunuliwa na mmiliki wake Sharon Voorhees kutoka kwenye duka la wanyama wa kufugwa akiwa na umri wa wiki sita.

Sharon alimnunua paka huyo kwa Dola za Marekani 10$ sawa na shilingi 21,000 za Tanzania.
 
Umri wa kadri wa paka ni miaka 12 hadi 15.
 
Marehemu paka Tiffany Two alievunja rekodi ya dunia kama paka mwenye umri mkubwa zaidi. Amekufa akiwa ni umri wa miaka 27.

Marehemu paka Tiffany Two alievunja rekodi ya dunia kama paka mwenye umri mkubwa zaidi. Amekufa akiwa ni umri wa miaka 27.

Mama Sharon Voorhees aliefiwa na paka wake mkongwe, nadhani yu na majonzi kwa sasa.

Monday, January 5, 2015

JAMAA MCHAFU KULIKO WOTE DUNIANI,HAJAOGA KWA MIAKA 60

#1.Kucha kama za Mnyama?

Unaweza usikubaliane nami kwamba kucha zake ni kama za mnyama,ona jinsi ngozi take inavyotisha,Je,unadhani amekuwa akikata kucha zake katika kkipindi hicho cha miaka 60? kwa sababu urefu wake haulingani na umri huenda zingekuwa ndefu zaidi.

#2. Sura ngumu!

Wakati tukimzungumzia babu wa miaka 80 ambae hajaoga kwa miaka 60 ilikuwa ni muhimu kwamba ukaona sura yake katika muonekano wa karibu zaidi, ili kufananisha atafananaje mtu ambae hatooga kwa miaka 60? Je, umegundua kuwa meno yake pia yameota kutu! hebu fikiria harufu itakayokuwa inatoka hapo dah!



#3. Kibaya zaidi ni mvutaji wa kiko!

Bwana huyu inaelezwa kuwa ni mvutaji mzuri,jape anachokivuta hakieleweki,lakini pia hicho kiko ni kikukuu na kichafu!


#4. Je,ni chakula au uchafu?

Sasa hapa ni zaidi ya uchafu kama hiki kinachoonekana ni chakula chake basi tumboni humo kazi kweli,lakini hapana shaka Mungu anamlinda!

#5. Malazi

Kwa malazi haya ni lazima awe mchafu

#6.  Hobi ya uvutaji au hitaji la muhimu,ukiambiwa sio chizi ni makusudi.

Awali tulimuona akivuta kiko sasa ni sigara nne kwa mpigo,si kawaida kwa binadamu wa kawaida kufanya haya lakini kwa huyu bwana hilo linawezekana.


#7. Baridi au jua kali?

Kwa sababu anaishi katika miamba na vilimani huenda anajisikia baridi, bwana huyu yu ana muonekano wa tofauti na binadamu wengine.!

Haya nido maisha dunia duara.

Dunia hii aisee in a mambo sana na wakati fulani inastaajabisha, kwa kuwa tumekuwa tukiona mambo kadha wa kadha ya kushangaza hata kuzidi KAWAIDA.

Leo Habarika kwa kushirikiana na Shirika la Habari la Iran IRNA tunakuonyesha picha na kukupa maelezo ya mtu mchafu zaidi duniani ambae ana umri wa miaka 80 na hajaoga kwa miaka 60! maajabu haya!

Babu huyu haijayumkinika bado kama ana matatizo ya akili ama laah! kwani amekuwa akizungumza na hata kufanya mambo mengine wanayofanya binadamu wenye utashi kamili.

Kwa namns nyingine anaweza hata kumchefua mtu kwa mtazamo wake

Ukimtazama katika picha napa chini NGOZI yake ina magamba, KUCHA zake ni ndefu na chafu, MENO take nod balsa jingine,zebu fikiria kama hajaswaki kwa miaka 60 harufu take itakuwaje.MACHO yake hayaoni vizuri kutokana na uchafu uliokithiri,HARUFU yake kwa waliomshuhudia wanasema ni mbaaayaaa sana!!!

Saturday, February 22, 2014

PRESS RELEASE KUTOKA TFF...MALINZI KUPATA USHIRIKIANO CAF

 Rais wa TFF, Jamal Malinzi akiwa na Rais wa CAF, Issa Hayatou na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF, Leodegar Tenga makao makuu ya CAF jijini Cairo, Misri.
                   

Release No. 029
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Februari 21, 2014

RAIS MALINZI AAHIDIWA USHIRIKIANO CAF
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemwahidi ushirikiano Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi.

Ahadi hiyo imetolewa leo (Februari 21 mwaka huu) makao makuu ya CAF jijini Cairo na Rais wa shirikisho hilo Issa Hayatou alipokutana na Rais Malinzi aliyekwenda kujitambulisha huko.

Utambulisho wa Rais Malinzi kwa Rais Hayatou uliongozwa na mtangulizi wake Leodegar Tenga ambaye aliiongoza TFF kwa vipindi viwili kuanzia 2004 hadi 2013.

Tenga ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), alimweleza Rais Hayatou kuwa uchaguzi wa TFF ulikuwa mzuri.

Aliongeza kuwa alimkabidhi kijiti Rais Malinzi kwa maridhiano na ana imani na uongozi wake.

Rais Hayatou alimpokea Rais Malinzi na kuahidi kuendelea kuipa Tanzania ushirikiano hasa katika maeneo ya utawala, ufundi na kuboresha miundombinu ya kuendeleza mpira wa miguu.

Kwa upande wake, Rais Malinzi alisema TFF itaendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa CAF ili kuhakikisha kiwango cha mpira wa miguu nchini Tanzania kinakuwa.

Baadaye mchana, Rais Malinzi alipata chakula cha mchana pamoja na wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji ya CAF.


Monday, December 23, 2013

KUTOKA TFF: MECHI YA MTANI JEMBE YAINGIZA MIL 422/-


Mechi ya Nani Mtani Jembe kati ya Yanga na Simba iliyochezwa juzi (Desemba 21 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 imeingiza sh. 422,611,000.

Mapato hayo ni kutokana na washabiki 52,589 waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 40,000. Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo walikuwa 19,044.

Asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa kutokana na mapato hayo ni sh. 64,466,084.75 wakati gharama za kuchapa tiketi ni sh. 7,488,000.

Mgawo mwingine ilikuwa kama ifuatavyo; kila klabu imepata sh. 117,470,066.61, asilimia 15 ya uwanja ni sh. 52,598,537.29, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 35,065,691.53 wakati gharama za mchezo zilikuwa sh. 28,052,553.22.

MALINZI, MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atakuwa na mkutano na waandishi wa habari utakaofanyika kesho (Desemba 24 mwaka huu).

Mkutano huo utafanyika saa 6 kamili mchana kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Friday, November 15, 2013

MAAFISA WAWILI WA TRA MBARONI SAKATA LA PEMBE ZA NDOVU ZA MABILIONI ZANZIBAR

Na Mohammed Mhina wa Jeshi la Polisi-Zanzibar
ZANZIBAR NOVEMBA 15, 2013. Jeshi la Polisi Zanzibar limewakamata watuhumiwa wemhine watatu wakiwemo Maafisa wawili wa Mamlaka ya Mapato nchini TRA kituo cha Bandari Zanzibar kwa kuhusika na kashfa ya kupatikana kwa meno ya tembo yenye thamani ya Mabilioni ya shilingi.
Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa, amewataja Maafisa hao wa TRA waliokamatwa kuwa ni Omari Hamad Ali(50) na Mohammed Hija(48) ambao wote wanafanyia kazi katika Bandari ya Zanzibar. Mtuhumiwa mwingine ni kibarua wa Mamlaka ya bandari Zanzibar Haidar Ahmad Abdallah(54).
Kukamatwa kwa watuhumiwa hao kunaifanya idadi ya watuhumiwa waliokamatwa hadi sasa kwa kuhusika na sakata hilo kufikia watano.
Kamishna Mussa amesema Watuhumiwa wengine wawili ambao ni wafanyakazi wa Kampuni ya Uwakala wa Mizigo ya Island Sea Food Limited, Mohammed Suleiman Mussa(45) na Juma Ali Makame(34) wao walikamatwa siku ya tukio la kukamatwa kwa meno hayo ya tembo kwenye Bandari ya Zanzibar.
Tayari watuhumiwa hao wamesafirishwa kwenda Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano zaidi. Pamoja na mambo mengine, kusafirishwa kwa watuhumiwa hao kwenda Jijini Dar es Salaam, kunatokana na Zanzibar kutokuwa na Sheria maalumu inayohusu wanyamapori. 
Maafisa wa Idara ya Wanyamapori nchini, leo wamekamilisha kazi ya kuhesabu na kulinganisha vipande 1,023 vya meno ya tembo vilivyokamatwa jana kwenye Bandari ya Zanzibar na kubaini idadi ya tembo waliouawa kuwa ni 305.
Meno hao yenye uzito wa kilo 2,915  yenye thamani ya Dolla 4,775,000 sawa na shilingi 7,480,125,000 za Tanzania (Bil.7.4), yalikamatwa juzi yakiwa yamehifadhiwa katika magunia 98 na kuwekwa kwenye konteina moja la futi 40 lenye namba PCIU 857619/0 lillilokuwa tayari kupakiwa kwenye meli ya MV Kota Henning kupelekwa nchini Ufilipino kwa magendo.
 Hadi sasa bado Makachero wa Polisi wa Kimataifa Interpol hapa nchini kwa kushirikiana na Makachero wa Polisi Zanzibar, idara ya wanyamapori makao makuu wanaendelea na upelelezi wa kuwabaini wale tote waliohusika na kashfa hiyo.
 
Jana Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa, alisema kuwa kazi kubwa iliyobaki ni kuhakikisha kuwa upelelezi wa kina unafanyika ili kuwakamata wale wote wanaohusika na mtandao huo.
Alisema hadi sasa Jeshi la Polisi bado linamsaka tajiri aliyewezesha mipango ya kukusanywa na kusafirisha shehena hiyo kutoka Tanzania Bara hadi Zanzibar ili kusafirishwa nje ya nchi.

Tuesday, November 5, 2013

MICHEZO:TANZANITE KWENDA MAPUTO KESHO + NYINGINE KADHAA ZA MICHEZO


  TFF  Release No. 190
ASHANTI UTD, SIMBA UWANJANI VPL
Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zinaanza kesho (Novemba 6 mwaka huu) ambapo Ashanti United itakuwa mwenyeji wa Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Viingilio katika mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 10 kamili chini ya mwamuzi Andrew Shamba kutoka Pwani ni sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Waamuzi wasaidizi ni Abdallah Mkomwa na Rashid Abdallah wote kutoka Pwani wakati mezani atakuwa Hamisi Chang’walu.

Mechi nyingine za kesho ni JKT Ruvu Stars na Coastal Union (Uwanja wa Chamazi), Kagera Sugar na Mgambo Shooting (Uwanja wa Kaitaba, Bukoba) na Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar (Uwanja wa Manungu, Morogoro).

Keshokutwa (Novemba 7 mwaka huu) raundi ya 13 kumaliza mzunguko wa kwanza itakamilika kwa mechi kati ya Yanga na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.

Azam itakuwa mwenyeji wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Chamazi wakati Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Rhino Rangers na Tanzania Prisons kutoka Mbeya.

Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City, Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Rhino itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons.

TFF YATAKA ORODHA YA WALIOSAMEHEWA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetuma waraka kwa vyama vya mpira wa miguu vya wilaya, mikoa na vyama shiriki kuvitaka kuwasilisha orodha ya wote waliofaidika na msamaha wa Oktoba 28 mwaka huu.

Oktoba 28 mwaka huu wakati akizungumza katika Mkutano Mkuu baada ya uchaguzi, Rais mpya wa TFF, Jamal Malinzi alitoa msamaha kwa wote waliofungiwa kwa sababu mbalimbali.

Hata hivyo, msamaha huo hauwahusu waliofungiwa kutokana na makosa ya rushwa au kupanga matokeo. Vilevile haugusi adhabu zilizotolewa ndani ya klabu.

Vyama vya mikoa vinatakiwa kuhakikisha waraka huo unafika kwa wanachama wao (vyama vya mpira wa miguu vya wilaya). TFF inataka orodha ya wote waliofaidika na msamaha huo kwa ajili ya kumbukumbu zake (records).

TANZANITE KWENDA MAPUTO KESHO
Kikosi cha timu ya Taifa ya wanawake chini ya miaka 20 (Tanzanite) kinaagwa kesho (Novemba 6 mwaka huu) saa chache kabla ya kuanza safari ya kwenda Maputo, Msumbiji.

Hafla fupi ya kuikabidhi bendera Tanzanite itafanyika kesho saa 5 asubuhi kwenye ofisi za TFF wakati kikosi hicho kinatarajiwa kupaa saa 11 jioni kwa ndege ya LAM na kuwasili Maputo saa 3.45 usiku.

Msafara wa Tanzanite ambayo ilishinda mechi ya kwanza mabao 10-0 karibu wiki mbili zilizopita jijini Dar es Salaam utaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Kidao Wilfred.

Mechi hiyo ya marudiano itachezwa Novemba 9 mwaka huu Uwanja wa Taifa wa Zimpeto, na timu itarejea nyumbani Novemba 10 mwaka huu saa 8.30 mchana kwa ndege ya LAM.

Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Thursday, October 31, 2013

JESHI LA POLISI: TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

Jeshi la Polisi Tanzania linawaita kwenye usaili wahitimu wa vyuo vya Elimu ya Juu na  vya Ufundi  Stadi ambao majina yao yanapatikana katika tovuti ya Jeshi la Polisi Tanzania, www.policeforce.go.tz
Orodha  ya majina hayo itapatikana  pia katika Gazeti la habari Leo la tarehe  04/11/2013.


Usaili utafanyika kuanzia tarehe 11/11/2003 hadi tarehe 15/11/2013 saa mbili asubuhi [02:00] hadi saa kumi jioni [10:00] kila siku kwa taaluma/fani na katika maeneo yafuatayo;


Fani za Menejimenti  ya Rasilimali Watu, Utawala, Uchumi, Usimamizi wa Sheria na Utekelezaji(BaLe), Ualimu, Sosholojia, Saikolojia na Ushauri Nasihi, Sheria, Takwimu, Lugha, Uhusiano wa Kimataifa, Uandishi wa habari na Mawasiliano ya Umma, Maendeleo ya Jamii, Ukutubi na Utunzaji Kumbukumbu. 


Usaili  wa fani hizi  utafanyika katika chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam(DPA) kilichopo kando kando ya barabara ya Kilwa Kurasini Dar es salaam .
Fani ya Udereva ,Ufundi rangi za magari(spray and Painting /Panel Beating ), Ufundi wa matengenezo ya Magari Makubwa(Auto-Mechanics-Heavy Duty) na Ufundi wa Matengenezo ya Umeme wa Magari(Auto Elecrical ). Usaili wa  fani hizi utafanyika Kikosi cha Polisi Ufundi kilichopo kando kando ya barabara ya Kilwa Kurasini Dar es salaam.
Fani za Kompyuta. Usaili wao utafanyika nyuma ya kikosi cha Ufundi yaani  TEHAMA KEKO chini.


Fani ya Uhandisi Mitambo(Mechanical Engineering ). Usaili wao utafanyika Kikosi cha Polisi Anga kilichopo Uwanja wa Ndege JK Nyerere DSM.


Wataalam wa masuala ya Afya/Wauguzi usaili wao utafanyika katika kikosi cha afya kilichopo kando kando ya barabara ya Kilwa Kurasini Dar es salaam.
   

Muhimu: 

(i)Mwombaji afike kwenye usaili akiwa na nakala  halisi  pamoja na vivuli vya  vyeti vyote vya Masomo/Taaluma [Academic Transcript (s)/Certificate(s)]yaani  kidato cha nne, sita ,Chuo na cheti cha kuzaliwa. Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika. 


(ii)Mwombaji aliyeitwa kwenye usaili atalipia gharama za upimaji afya shilingi elfu kumi (10,000), usafiri, chakula na malazi kwa muda wote wa zoezi la usaili. 


(iii)Kwa kuwa muda ni mchache anaekuja kwa usaili ajiandae baada ya usaili atakaechaguliwa atapelekwa katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi siku nne baada ya usaili kwisha yaani tarehe 19/11/2013.