Thursday, October 31, 2013

JESHI LA POLISI: TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

Jeshi la Polisi Tanzania linawaita kwenye usaili wahitimu wa vyuo vya Elimu ya Juu na  vya Ufundi  Stadi ambao majina yao yanapatikana katika tovuti ya Jeshi la Polisi Tanzania, www.policeforce.go.tz
Orodha  ya majina hayo itapatikana  pia katika Gazeti la habari Leo la tarehe  04/11/2013.


Usaili utafanyika kuanzia tarehe 11/11/2003 hadi tarehe 15/11/2013 saa mbili asubuhi [02:00] hadi saa kumi jioni [10:00] kila siku kwa taaluma/fani na katika maeneo yafuatayo;


Fani za Menejimenti  ya Rasilimali Watu, Utawala, Uchumi, Usimamizi wa Sheria na Utekelezaji(BaLe), Ualimu, Sosholojia, Saikolojia na Ushauri Nasihi, Sheria, Takwimu, Lugha, Uhusiano wa Kimataifa, Uandishi wa habari na Mawasiliano ya Umma, Maendeleo ya Jamii, Ukutubi na Utunzaji Kumbukumbu. 


Usaili  wa fani hizi  utafanyika katika chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam(DPA) kilichopo kando kando ya barabara ya Kilwa Kurasini Dar es salaam .
Fani ya Udereva ,Ufundi rangi za magari(spray and Painting /Panel Beating ), Ufundi wa matengenezo ya Magari Makubwa(Auto-Mechanics-Heavy Duty) na Ufundi wa Matengenezo ya Umeme wa Magari(Auto Elecrical ). Usaili wa  fani hizi utafanyika Kikosi cha Polisi Ufundi kilichopo kando kando ya barabara ya Kilwa Kurasini Dar es salaam.
Fani za Kompyuta. Usaili wao utafanyika nyuma ya kikosi cha Ufundi yaani  TEHAMA KEKO chini.


Fani ya Uhandisi Mitambo(Mechanical Engineering ). Usaili wao utafanyika Kikosi cha Polisi Anga kilichopo Uwanja wa Ndege JK Nyerere DSM.


Wataalam wa masuala ya Afya/Wauguzi usaili wao utafanyika katika kikosi cha afya kilichopo kando kando ya barabara ya Kilwa Kurasini Dar es salaam.
   

Muhimu: 

(i)Mwombaji afike kwenye usaili akiwa na nakala  halisi  pamoja na vivuli vya  vyeti vyote vya Masomo/Taaluma [Academic Transcript (s)/Certificate(s)]yaani  kidato cha nne, sita ,Chuo na cheti cha kuzaliwa. Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika. 


(ii)Mwombaji aliyeitwa kwenye usaili atalipia gharama za upimaji afya shilingi elfu kumi (10,000), usafiri, chakula na malazi kwa muda wote wa zoezi la usaili. 


(iii)Kwa kuwa muda ni mchache anaekuja kwa usaili ajiandae baada ya usaili atakaechaguliwa atapelekwa katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi siku nne baada ya usaili kwisha yaani tarehe 19/11/2013.

No comments:

Post a Comment