Release No. 014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Januari 27, 2013
PAMBANO LA LYON, SIMBA LAINGIZA MIL 53/-
Mechi
namba 92 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa jana (Januari 27 mwaka huu)
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Simba kuibuka na
ushindi wa mabao 3-1 limeingiza sh. 53,756,000.
Watazamaji
9,408 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa kwa viingilio
vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu
ikipata mgawo wa sh. 12,499,752.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT) iliyolipwa ni sh. 8,200,067.80.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 6,355,806.33,
tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 3,813,483.80, Kamati ya Ligi
sh. 3,813,483.80, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
1,906,741.90 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 1,483,021.48.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment