TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 28. 01.2013.
WILAYA YA MBEYA MJINI - KUPATIKANA NA
BHANGI.
MNAMO
TAREHE 27.01.2013 MAJIRA YA SAA 14:00HRS HUKO ENEO LA UYOLE JIJI NA MKOA WA
MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA ASAM S/O JOHANUS,MIAKA
24,KYUSA,MKULIMA MKAZI WA MTAA WA MWANYANJE – UYOLE AKIWA NA BHANGI YENYE UZITO
WA KILO 1 NA GRAM 400. MBINU ILIYOTUMIKA NI UPEKUZI. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MVUTAJI WA BHANGI. TARATIBU
ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI MTUHUMIWA AFIKISHWE
MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI
ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME
CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Signed By,
[DIWANI ATHUMANI – ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment