DODOMA JUMAMOSI 16.06.2012
Kampuni lililofanya Utafiti wa Gesi |
Taarifa
hiyo imetolewa (leo Jumamosi 16.06.2012) na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya ugunduzi wa
gesi asilia katika mwambao wa Mikoa ya Mtwara na Lindi.
Profesa
Muhongo amesema kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita kumekuwepo
kasi kubwa ya utafutaji wa mafuta na gesi asili hapa nchini.
Amesema
kuwa utafiti huo umejikita zaidi kwenye bahari ya Hindi kwenye maji ya
kina kirefu,kiasi cha gesi iliyogundulika katika kina cha maji marefu
inafikia takribani futi za ujazo trioni 20.97 ikiwa imejumuisha kisima
kilichogunduliwa wiki hii cha Lavani.
Waziri
huyo alizitaja Kampuni zilizohusika na utafiti wa gesi asili kuwa ni
Kampuni ya Statoil ya Norway kwa kushirikiana na Kampuni ya Exxon Mobil
ya Marekani zimegundua na kuthibitisha kuwepo kwa gesi asili yenye futi
za ujazo 20.97 katika kisima cha Lavana katika kitalu Na.2 Mashariki mwa
Lindi.
Aidha
alisema kisima kilichochimbwa Songo Songo Kisiwani na kukamilika Mei
mwaka huu kimegunduliwa kuwa na uwezo wa kuzalisha futi za ujazo milioni
60 kwa siku.
Pwani ya Lindi na Mtwara ambako Gesi imepatikana |
Hata
hivyo alisema pamoja na kuwa utafiti wa gesi asili umeonyesha kuwa na
gesi nyingi lakini utafiti wa mafuta na gesi kwenye bahari ya kina
kirefu unagharimu fedha nyingi, alieleza kuwa kisima kimoja takribani
Dola za Marekani milioni 100 hadi 150 baada ya gharama za kukusanya
takwimu za mitetemo.
Alisema
kutokana na upatikanaji wa gesi asilia ya kutosha itawwezesha serikali
kuwa na uhakika wa matumizi ya nisshati ya umeme na kuepukana na
matumizi ya kuni na mkaa.
“Baada
ya mika mitatu ijayo gesi asilia itaweza kutumiwa na watanzania wengi
ikiwani ni pamoja na watumiaji wa majumbani na kuepukana na matumizi ya
mkaa na kuni”alisema Profesa Muhongo.
No comments:
Post a Comment