Tuesday, January 3, 2012

APANDISHWA KIZIMBANI KWA KUIBA LAPTOP YA HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA

Imeandikwa na : Msafiri Njilamhaja, Mbeya

Mahakama ya Hakimu Mkazi Jijini Mbeya imempandisha Kizimbani ROBERT MWANZUNJE (51) Mkazi wa Kalobe Jijini Mbeya kwa kosa la wizi wa Kompyuta aina Laptop mali ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya
Kielelezo: Sheria

Akisoma Mashtaka katika Mahakama hiyo Mwendesha Mashtaka wa Serikali BASSILUS NAMKAMBE mbele ya Hakimu Mkazi MONIKA NDYEKOBORA amesema mnamo Tarehe 16/12/2011 katika ofisi za Halmashauri ya Jiji la Mbeya Mtuhumiwa akiwa kama mtumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya aliiba Laptop yenye thamani ya shilingi za Tanzania Milioni moja na Laki Saba na Nusu Kompyuta ambayo ni Mali ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya

Imeelezwa Mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka  kuwa Mtuhumiwa amefanya kosa hilko kinyume na kifungu cha Sheria nambari 271 cha Kanuni za adhabu Sura nambari 16 kama kilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002

Baada ya Mtuhumiwa kusomewa Shtaka linalomkabili amekana kuhusika na kosa hilo na Hakimu Mkazi amepanga masharti ya dhamana ambapo Mtuhumiwa ametakiwa kutafuta wadhamini wawili wakiwa na kiasi cha fedha shilingi milioni moja vitambulisho vya Uraia pamoja na barua kutoka kwa Mtendaji wa Kijiji au Kata kikionyesha uhalali wa Makazi ya Wadhamini hao

Hata hivyo Mtuhumiwa amerudishwa Korokoroni kutokana na Wadhamini kushindwa kutimiza masharti yaliyotolewa na mahakama hiyo, Shauri hilo limeahirishwa hadi Januari 16 litakapotajwa tena Mahakamani hapo

No comments:

Post a Comment