Na:Mwandishi Maalum (Dodoma)
MSANII wa Vichekesho nchini Masanja Mkandamizaji amewataka wasomi kuhakikisha wanajikita katika masomo badala ya kujiingiza katika anasa ambazo haziwezi kuwasaidia hapo baadaye.
Kauli hiyo ameitoa hivi karibuni katika tamasha la uzinduzi wa Albamu ya Yesu Unaweza ambayo imeimbwa na mama Mchungaji wa Kanisa la Calvary Josephine Kihoza ambayo ilizinduli katika ukumbi wa chuo kikuu cha St John’s Mjini Dodoma
Masanja amesema kuwa wasomi wengi wawapo vyuoni hujisahau na badala ya kujikita katika masomo yao wanajiingiza katika masuala ya anasa jambo ambalo jamii inashindwa kuwapambanua na wale ambao si wasomi.
Mbali na hilo alisema ili mtu aweze kulifanya jambo lolote la ambalo lina tija katika jamii na taifa ni lazima watamzania wakajenga tabia ya uaminifu na uadilifu.
Msanii huyo amabye kwa sasa amejikita katika nyimbo za injili pia aliwataka wanavyuo kuachana na tabia ya kubeza kazi ya mungu na badala ya kumtukuza shetani ni bora sasa wakamtumikia mungu kwa nguvu zote.
Akiongea kwa sauti ya usanii Masanja alisema “ Jamani nyinyi wasomi chonde chonde tunawategemea lakini mbona hamueleweki mnajifanya wasomi lakini mbona mnamkasilisha mungu wenu.
“Nataka kuwaambia masomo bila mungu ni kazi bure, pia kazi bila hofu ya Mungu ni fujo kwani ni lazima kuwepo na uadilifu na uaminifu katika utendaji wa kazi katika maeneo yoyote” alisema Masanja.
Kwa upande wake mama mchungaji, Josephine Kihoza alisema kuwa pamoja na kumtumikia mungu kwa njia ya uimbaji pia anakusudia kuwasaidia watoto waishio katika mazingira pamoja na wale yatima.
Aidha aliwataka waimbaji wa nyimbo za injili kuhakikisha wanatunga nyimbo ambazo zinalenga kuwafariji na kuwatia matumaini wasikilizaji wa nyimbo hizo badala ya kuimba nyimbo kwa malengo ya kujifurahisa.
Msanii maarufu nchini Masanja Mkandamizaji akitumbuiza katika uzinduzi wa Albamu ya mama mchungaji Josephine Kihoza albamu hiyo inaitwa 'Yesu Anaweza'. |
Katika tamasha hilo mgeni rasm alikuwa ni mbunge wa Kibakwe Simba Chawene (CCM) na alifanikisha kukusanya kiasi cha shilingi zaidi ya milioni tano ambazo zitaelekezwa katika kuwasaidia watoto waishi katika mazingira magumu kama ilivyo kusudiwa na mwimbaji huyo.
Mbunge huyo pekee alichangia kiasi cha shilingi milioni 3, pia aliwataka wana siasa nchini kujijengea tabia ya kutoa mali zao kwa ajili ya kazi ya mungu badala ya kutumia mali zao bila mpangilio.
“ Wana siasa wenzangu ni bora kutumia fedha zenu kwa ajili ya kumtumikia Mungu na kuisaidia jamii lakini wapo wanasiasa ambao wanatumia mali zao kwa ajili ya mambo ya anasa jambo ambalo ni chukizo mbele za mungu” alisema Simbachawene.
No comments:
Post a Comment