Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi Diwani Athumani |
Wilaya ya momba - kuvunja chumba cha
guest mchana na kuiba
Mnamo
tarehe 24.01.2013 majira ya saa 10:30hrs huko katika nyumba ya kulala wageni
iitwayo serengeti iliyopo tunduma wilaya ya momba mkoa wa mbeya. Joyce d/o
kemto,miaka 38,mfanyabiashara,mkisii mkazi na raia wa nchini kenya aliyekuwa
amepanga katika chumba no.06 aliibiwa pesa tshs 150,000/= zilizokuwa kwenye
mkoba ndani ya chumba hicho. Watuhumiwa wawili 1.emanuel s/o charles, miaka 40, mzanaki, mkulima mkazi wa magomeni
dsm na 2. Godfrey s/o benard @ simfukwe,miaka
42,muha,mkulima mkazi wa mwandiga kigoma wamekamatwa wakiwa na mkoba wenye pesa
hizo. Mbinu iliyotumika ni kupanga chumba jirani na mhanga na kisha kufungua
mlango wa chumba kwa kutumia funguo bandia wakati mhanga akiwa nje. Mhamga
alipiga kelele za kuomba msaada baada ya kuwaona watuhumiwa wakiwa na mkoba
wake na ndipo wananchi walipoanza kuwashambulia kwa kuwapiga mawe na fimbo hata
hivyo walitokea askari polisi na kuwaokoa. Mtuhumiwa godfrey s/o benard @ simfukwe hali yake ni mbaya amelazwa kituo cha
afya tunduma na mwenzake anaendelea kushikiliwa polisi. Taratibu za kisheria
zinafanywa ili wafikishwe mahakamani. Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna
msaidizi wa polisi diwani athumani
anaendelea kutoa wito kwa jamii kuacha kujichukulia sheria mkononi
na pindi wanapowakamata wahalifu na
badala yake kuwafikisha katika mamlaka husika ili sheria ichukue mkondo wake.
Aidha anatoa rai kwa wamiliki wa nyumba za kulala wageni kuimarisha ulinzi muda wote katika biashara zao. Pia
anawakumbusha kutoa taarifa haraka mamlaka husika juu ya mtu/watu
wanaowatilisha shaka ambao wanafika kama
wateja ili hatua dhidi yao zichukuliwe.
Wilaya ya kyela - kuingia nchini bila
kibali.
Mnamo
tarehe 23.01.2013 majira ya saa 17:00hrs huko katika kijiji cha ibanda wilaya
ya kyela mkoa wa mbeya. Polisi waliwakamata watu watano raia wa nchini burundi
wakiwa wameingia nchini bila kibali ambao ni {1}.alakeza s/o mose,miaka 32 {2}.
Bulalahubwa s/o kalodati, miaka 25 {3}. Alakazya s/o alini, miaka 6 {4}. Nishuna d/o dorina, miaka 6, na {5}. Munyeze d/o jozina, miaka 9 . Mbinu iliyotumika ni kusafiri kwa
njia ya kificho na kukutwa katika kanisa la babtisti kijijini hapo wakiomba
hifadhi. Watuhumiwa wamekabidhiwa idara ya uhamiaji. Kamanda wa polisi mkoa wa
mbeya kamishna msaidizi wa polisi diwani athumani anatoa wito kwa jamii
kuendelea kutoa taarifa kwa mamlaka husika juu ya mtu/watu wanaowatilia shaka
ikiwa ni pamoja na wahamiaji haramu.
Wilaya ya mbozi - kusalimishwa kwa
silaha moja aina ya gobole
Mnamo
tarehe 23.01.2013 majira ya saa 06:00hrs huko katika kijiji cha iyula wilaya ya
mbozi mkoa wa mbeya. Mtu/watu wasiofahamika walisalimisha /telekeza bunduki
moja aina ya gobole yenye namba – towkk 340. Mbinu iliyotumika ni
kutelekeza silaha hiyo jirani na kituo
kidogo cha polisi iyula na polisi
kuichukua . Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi wa polisi diwani
athumani anatoa wito kwa jamii kuwafichua kwa kutoa taarifa juu ya mtu/watu
wanaomiliki /tengeneza silaha bila kibali ili hatua za kisheria zichukuliwe
dhidi yao. Aidha anatahadharisha wamiliki/watengenezaji haramu wa silaha hizo
kuzisalimisha haraka ingawa muda wa “offer” umemalizika kuliko kusubiri
kukamatwa.
Wilaya ya chunya - kupatikana na bhangi
Mnamo
tarehe 24.01.2013 majira ya saa 18:56hrs huko katika kijiji cha nzigwa wilaya
ya chunya mkoa wa mbeya. Askari polisi wakiwa doria waliwakamata 1.makenza s/o igembe, miaka 45,
msukuma, mkulima na 2. Milembe d/o mala,miaka
65,msukuma mkulima wote wakazi wa kijiji cha nzigwa wakiwa wanamiliki shamba la
bhangi lenye ukubwa wa nusu ekari .
Watuhumiwa ni wakulima na wauzaji wa bhangi. Bhangi yote imeteketezwa kwa
kuchomwa moto shambani. Taratibu zinafanywa ili watuhumiwa wafikishwe
mahakamani. Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi wa polisi diwani
athumani anatoa wito kwa jamii kuacha tumia dawa za kulevya kwani ni kinyume
cha sheria na ni hatari kwa afya ya mtumiaji. Aidha anatoa rai kwa mtu/watu
wenye taarifa juu ya wamiliki na mahali yalipo mashamba ya bhangi kuzitoa kwa
mamlaka husika ili hatua dhidi ya wahusika zichukuliwe.
Signed by,
[diwani athumani – acp]
Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya.
No comments:
Post a Comment