Friday, January 25, 2013

SAKATA LA GESI ASILIA MTWARA WANANCHI WATUMIA GHARAMA KUHAMASISHANA...WASEMA ITAFIKA DAR IKIWA 'MAJI' !!

Mkazi wa Mtwara akionyesha Fulana inayodhihirisha msimamo wa Wana-Mtwara kuhusu Gesi.PICHA NA: ROSINA

Sakata la Gesi Mkoani Mtwara limechukua sura mpya baada ya wananchi kuingia mifukoni na kuhamasishana ili kuhakikisha gesi asilia ambayo imepatikana Mkoani humo haisafirishwi kwenda jijini Dar es Salaam

Baadhi ya Wananchi hao wakizungumza na Mwandishi wa HABARIKA wamesema kuwa hawataki 'kuchezewa' juu ya suala hilo na wanaitaka serikali iwasikilize

''Tunahitaji maelewano kuhusu suala hili hatutaki serikali ifanye siasa kwenye suala hili, sisi si watu wa kuchezewa, hapa haitoki gesi wala nini'' alinukuliwa mmoja wa wananchi.

Wakati hayo yakijiri   Bibi Somoye Issa (90) ambaye ni 'Bibi wa Mtaa' katika kijiji cha Msambati ametoa kitisho kwa serikali na kusema kuwa iwapo Gesi hiyo itasafirishwa kwenda Dar es salaam basi itafika huko ikiwa maji!


Bibi Somoye Issa (90).

Bibi huyo mkazi wa Kijiji cha Msimabati ambako gesi asilia hiyo ndiko imegundulika amesema sayansi ya asili itashindana na ya kisasa ili kuhakikisha gesi hiyo haifiki Dar es salaam na kutumiwa kama serikali ilivyodhamiria    
                                                                                                   Mapema gari lililokuwa limeandaliwa kumbeba bibi huyo ili kusaidia mchakato wa kufanya zindiko lilikutwa likiwa limeungua moto, il hali chanzo cha ajali hiyo ya kuungua kwa gari hilo kikiwa bado hakijulikani. 
Mhariri wa Blogu ya Kusini akiangalia gari hilo lililoteketea kwa moto.PICHA JAMII FORUM.

Mapema akihojiwa katika kipindi cha Dakika Arobaini na Tano kinachorushwa na ITV  Waziri wa Nishati na Mdini Prof. Sospeter Muhongo alisema kuwa suala la gesi halipaswi kuwa ni la watu wa Mtwara pekee kwani gesi hiyo ni mali ya watanzania wote

Kwa mujibu wa Shirika la Petroli nchini TPDC kiasi cha  futi za ujazo trilioni 35 zimepatikana na zaidi zinatarajiwa kupatikana.
 
 Katika kile kinachoonekana kuwa ni hatari, asubuhi ya leo tumepata taarifa kwamba gari lililoenda kwa ajili ya kumbeba Bibi kwenda naye kusikojulikana limechomwa moto. Taarifa zinasema, watu kadhaa akiwemo kijana mmoja mwenye asili ya ukaazi wa kijiji hicho walikamatwa jana usiku na wanakijiji cha Msimbati wakidai wameagizwa kuja kumchukua Bibi huyo ili wakafanye maongezi na Wakubwa ambao pia hawakuweza kuwekwa bayana ni Wakubwa gani hao. Kinachoelezwa ni kwamba, baada ya mtafaruku huo, watu hao walichoropoka na kukimbia kitu kilichowapa hasira wananchi na kuamua kuchoma gali hilo ambalo walikuja nalo.Pichani ni Wananchi wakiangalia mabaki ya gari hilo. JAMII FORUM

 

   






No comments:

Post a Comment