Dodoma Jan 21 2013
MWANAFUNZI
wa chuo kikuu cha mtakatifu Yohana
Lyidia Mzima (57) Mlugulu, ameuwawa na kunyofolewa nyama kwenye paja la mguu wa
kulia, karibu na eneo la chuo, na watu wasiojulikana wakati akitokea kujisomea
nyakati za usiku ambapo inasadikiwa pia kuwa alibakwa.
Akizungumza na
waandishi wa habari kamanda wa polisi wa mkoa wa Dodoma kamishina msaidizi, David
Misime lisema kuwa tukio hilo lilitokea jana usiku na kwamba mwanafunzi huyo
alikuwa akisoma fani ya uuguzi mwaka wa tatu chuoni hapo..
Alifafanua
kuwa mwili wa marehemu umegunduliwa asubuhi na wananchi ambao walijuliijulisha polisi
kuhusiana na tukio hilo ambao nao walifatilia na kubaini kuwa tukio hilo ni la
kweli.
Misime
alisema mwili huo ulikutwa ukiwa na jereha kichwani linaonyesha kusababishwa na
kitu chenye ncha kali, pia amekutwa na jeraha la kunyofolewa nyama kwenye paja
la mguu wa kulia.
“Marehemu
pia amekutwa amenyofolewa nyama kwenye mguu wake wa kulia sasa bado
haijafahamika kama amefolewa na fisi ama gani, mana mpaka sasa mnyama huyo
hajafahamika”,alisema misime.
Alisema
mwanafunzi huyo alikuwa amepanga nyumba mtaa wa kibaoni-Image B kata ya kikuyu
kusini ambapo inadaiwa kuwa aliwaaga wenzake aliokuwa akisoma nao majira ya saa
nne usiku tarehe 20 januari mwaka huu kuwa anarudi alikokuwa akiishi.
“Rafiki yake
waliyekuwa wanasoma pamoja ambaye
alikuwa kwenye msiba anaeleza kuwa
marehemu Lyidia alimpigia simu usiku huo wa jana akimuuliza kama amesharudi nyumbani
akamweleza bado, ambapo rafiki yake huyo anadai kuwa mara nyingi huwa analala
kwake”,alifafanua Kamanda huyo.
Kufuatia
tukio hilo la kusikitisha na kustusha kamanda misime alisema msako mkali wa
kuwatafuta wauaji ama muuaji unaendelea ili kuweza kuwabaini mara moja na
kuchukuliwa hatua stahiki.
“T ukio hili
hatutalifumbia macho tunafanya msako mkali mara moja na kuhakikisha wahusika
wanabainika na kuchukuliwa hatua ili iwe fundisho kwa wengine , natoa rai kwa
watu wanaojihusisha na vitendo hivi vya uharifu na mauaji kuacha mara moja kwa
jeshi la polisi halijalala kama wanavyofikili lipo kazini wakati wote.
Aidha
laisema wanaendelea kuimarisha doria na vikundi vya ulinzi shirikishi ambavyo
vitaendeshwa na wananchi wakiwemo wanachuo katika maeneo yao ili kulisaidia
jeshi la polisi katika kuthibiti matukio ya aina hiyo.
Kamishna
Misime alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia
maiti hospitali ya rufaa iliyopo mkoani hapa ukisubiri uchunguzi wa madaktari.
Pia misime
alisema wanakabiliwa na changamoto kubwa ya uchache wa askari polisi mkoani
hapa licha ya kuwepo kwa juhudi kubwa za kufanya doria za mara kwa mara katika
maeneo yote ya mkoa huu, hali ambayo imetokana na kupanuka kwa kasi kwa mji
huu.
Wakati
huohuo Tanzania daima imefanikiwa kufika eneo la tukio na kushuhudia mwili wa
marehemu Lyidia ukiwa katika eneo hilo la njia panda ya chuo hicho ukionyeshwa
marehemu akiwa ametolewa macho, dalili za kubakwa, majeraha mablimbali katika
eneo la kichwani na kwenye paja ambayo yote haya yanasubiriwa kudhibitishwa na
madaktari kama yametokana na nini.
Mmoja wa
wanafunzi aliyejulikana kwa jina la Baraka Gongo ambaye anasoma fani ya ualimu mwaka
wa tatu katika chuo hicho aliiambia Tanzania daima kuwa tukio hilo ni
kusikitisha sana na linaashilia upotevu wa amani kwa wanafunzi chuoni hapo.
“Tunaliomba
jeshi la polisi kutuimarishia ulinzi maana hapa tunasoma bila amani kwani hili
sio tukio la kwanza kutoa na kamanda aliyepita Zelothe aliahidi tutajengewa
kituo cha polisi ili ulinzi uwepo wakati wote lakini mpaka sasa hawajafanya
hivyo”,alisema Gongo.
Matukio ya
kubakwa, kulawitiwa, kuuwawa na kuibiwa kwa wanafunzi wa chuo yameendelea
kushamiri hapa nchini ikiwemo mkoani Dodoma hali ambayo inahatarisha amani ya
wanafunzi.
Mwisho
No comments:
Post a Comment