Monday, January 21, 2013

Azam FC kumaliza na KCB FC kesho Nairobi


NAIROBI
 
Timu ya Azam FC kesho Jumanne itamalizia ziara yake ya mechi za kirafiki jijini Nairobi kwa kucheza dhidi ya K.C.B kwenye Uwanja wa City.

Azam FC iko jijini hapa kwa ziara ya maandalizi kwa ajili ya ligi kuu na mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, imecheza michezo miwili, imefungwa 2-1 na AFC Leopards na ikashinda mchezo mmoja 1-0 SOFAPAKA.

Ziara hiyo ya siku saba inamalizika leo kwa mchezo huo ambapo kikosi hicho kitarejea jijini Dar es Salaam, siku ya Jumatano tayari kwa mechi za ligi kuu.

Katika ziara hiyo hadi jana jioni wachezaji wote walioko safarini wamecheza katika michezo hiyo miwili akiwepo kipa namba mbili Aishi Salum.

Akizungumzia mchezo wake wa mwisho, kocha Stewart alisema wachezaji wote wako safi kwa mchezo huo kwa  kuwa hakuna majeruhi yoyote katika michezo hiyo.

Alisema wakimaliza mashindano hayo watakuwa wamejiimarisha vya kutosha kwa ligi kuu, wachezaji watakuwa imara na kurekebisha makosa yao.

“Mechi na KCB tutacheza tukiwa safi, tumepumzika siku moja, wachezaji wamepata mapumziko, itakuwa mechi nzuri” alisema Stewart.

Mchezo huo utachezwa kwenye kiwanja cha City ambacho ni cha nyasi bandia sawa na kile cha Azam Complex Chamazi.

Mwisho

Azam FC 1-0 SOFAPAKA, Aishi aonesha kiwango cha juu

Goli pekee la mshambuliaji Gaudence Mwaikimba wa Azam FC, limeipa ushindi timu hiyo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya SOFAPAKA uliochezwa jana Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi, Kenya.

Azam FC imecheza mchezo wake wa pili wa kirafiki, juzi jioni walifungwa 2-1 na AFC Leopard katika mechi iliyochezwa uwanja huo.

Katika mchezo huo, kipindi cha kwanza kilimalizika kwa timu zote kutoka suluhu, wachezaji wa Azam FC Himid Mao alipiga mpira wa adhabu uliogonga mwamba na kurudi ndani katika dakika ya 14, dk 22 Seif Abdalah akiwa na lango la SOFAPAKA alipiga mpira uliotoka nje.

Azam FC waliendelea kufanya amshambulizi katika lango la SOFAPAKA, dk 27 na 45 Michael Bolou alipiga shuti likatoka nje na dakika ya 37 Humprey Mieno alishindwa kufunga na badala yake shuti likaokolewa na kipa wa SOFAPAKA, Duncan Ochieng

SOFAPAKA dk 24 Kago Dawson alikosa nafasi ya wazi kwa kupiga shuti lililodakwa vyema na kipa chipukizi wa Azam FC, Aishi Salum ambaye aliweza kulinda lango hilo katika vipindi vyote.

Kipindi cha pili Azam FC walifanya mabadiliko walitoka Samih Haji Nuhu, Michael Bolou, Khamis Mcha na David Mwantika nafasi zao zikachukuliwa Luckson Kakolaki, Abdulhalim Humud, Gaudence Mwaikimba na Malika Ndeule,mabadiliko hayo yaliimarisha kikosi hicho na kufanya mashambulizi mengi.

Kipa Aishi Salum alitumia vema nafasi aliyoipata katika mchezo huo kwa kuzuia mashuti ya wachezaji wa SOFAPAKA na kusimama vema katika nafasi hiyo, kutokana na umri wake mdogo amecheza katika kiwango cha juu kama anavyokuwa golikipa namba moja Mwadini Ally ambaye jana alipumzishwa na kuwapisha vijana Aishi na Jackson Wandwi.

Azam FC walipata goli katika dakika ya 58 kupitia kwa mkwaju wa penati iliyopigwa na Mwaikimba baada ya beki wa SOFAPAKA Kisuya Colins kunawa mpira katika eneo la hatari.

Goli hilo lilidumu hadi kumalizika kwa mchezo huo na kuifanya Azam FC kushinda 1-0 katika mchezo huo ulioshuhudiwa na Raisi wa SOFAPAKA, Elly Kalekwa na Katibu Mkuu wa Azam FC, Nassor Idrissa.

Azam FC kesho itapumzika na kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa City ambao watacheza siku ya Jumanne dhidi ya K.C.B na kumalizia safari hiyo ya mechi za kirafiki ikiwa ni maandalizi kwa ajili ya ligi kuu na Mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Azam FC, Aishi Salum, Himid Mao/Omary Mtaki, Samih Haji Nuhu/Luckson Kakolaki, Jockins Atudo, David Mwantika/Malika Ndeule 45’, Michael Bolou/Abdulhalim Humud 45’, Humphrey Mieno/Ibrahim Mwaipopo 66’, Salum Abibakar, Brian Umony Jabir Aziz 81’, Seif Abdalah/Uhuru seleman 68’, Khamis Mcha/ Gaudence Mwaikimba.

SOFAPAKA  Duncan Ochieng/Okeko David, Shivash Collins, Kisuya Collins, Situma James, Felly Mulumba, Abdalah Nyanzi, Hilary Echesa, Koko Manopi, Kagogo Patrick/George Owino, Kago Dawson na John Baraza/Tarumbwa Cabadian.
Mwisho

No comments:

Post a Comment