BUNGE KUANZA MKUTANO WA KUMI KESHO HUKO DODOMA; HOJA YA GESI MTWARA KUTAWALA
MKUTANO
wa kumi wa Bunge la kumi unatarajiwa kuanza jumanne hii January 28 2013 mjini Dodoma
huku sakata la gesi ya Mtwara,vitendo vya ujangili na mauaji holela ya
raia zikiwemo vurugu katika vyuo Vikuu yakiwa miongoni mwa mambo ambayo
yanatarajiwa kupewa kipaumbele katika mijadala.
Katika kikao cha kwanza cha mkutano wa kumi hakuna shughuli nzito
inayotarajiwa kufanyika zaidi ya kipindi cha maswali na majibu na baada
ya hapo kamati ya uongozi itakaa kupanga ratiba kamili ya Bunge.
Licha ya hatma ya sakata la
gesi ambayo inasubiriwa kwa shauku na mamilioni ya watanzania pia suala
la ujangili nalo linadaiwa kugeuka mwiba mchungu kutokana na
kuwanufaisha wachache kwa njia za panya.
Hivi karibuni
kumeripotiwa mauaji ya raia katika maeneo mbalimbali nchini sanjari na vurugu
katika vyuo vikuu ambazo nazo zimeacha sintofahamu miongoni mwa
wanafunzi huku wengine wakilazimika kukatisha masomo kwa hofu ya
kuhatarisha usalama wa maisha yao.
Mkutano wa kumi unatarajiwa kuahirishwa februari 8 mwaka huu endapo ratiba haitabadilika.
STAR TV
No comments:
Post a Comment