Thursday, December 6, 2012

WANASAYANSI WASTAAJABISHWA NA MAWE YANAYOTEMBEA



Alhamisi,December 6, 2012

Na: Shannon Dybvig

Wanasayansi nchini Marekani(Califonia) katika 'Bonde la Kifo' wameripoti kuwepo mawe ya ajabu yanalotembea uthibitisho unaodhihirishwa na ramani za matembeo ya mawe hayo katika eneo la jangwa lenye mchanga unaoonyesha 'matembeleo' ya mawe hayo.

Wanasayansi wa Marekani wanaoshughulikia masuala ya Miamba 'Geologists' wanasema hali hii inaweza kufananishwa na kutembea kwa mawe katika kina cha chini sana cha Bahari ambako mawe huru (Matumbawe Huru) hutembea kwa umbali mrefu kutokana na nguvu ya mvutano ndani ya maji.

Hata hivyo wanasayansi hao wamesema hawana uhakika ni nguvu gani ya mvutano ambayo imekuwa ikisababisha mawe hayo kutembea, huku wakibashiri kuwa huenda ni upepo,hali ya mvua na unyevunyevu.

Hebu yatazame mawe yenyewe katika picha zifuatazo:


Mawe haya yanayotembea si madogo.Mengi yana ukubwa wa Mkate. Picha na:Sandy Redding


Picha ya Juu inaonyesha Bonde la Kifo la Racetrack Playa linaloonekana katika umbo la Flampeni. Picha na: Kittell
Mawe hata yana uwezo wa kutembea hadi futi 1,500. Kinachostaajabisha zaidi ni kwamba unaweza ukaifuata njia ya mawe haya mwishowe usilikute jiwe.Picha na:NASA


Inayumkinika kuwa Mvua,Barafu,Umande na Upepo mkali vinayasaidia mawe haya kutembea.Matukio haya yamekuwa yakiripotiwa zaidi wakati wa Tufani. Picha na: Arno Gourdol



Mawe haya yamekuwa yakitengeneza njia za namna mbalimbali. Picha na: NASA


Mawe haya kwa mujibu wa wanasayansi wa Marekani yanapasuka kutoka katika Milima iliyo jirani na Bonde hilo la Kifo.Picha na: Sarah Katrina

1 comment: