Mmoja wa wakazi wa eneo akiwa pembeni ya hema kuukuu.Picha,Danson Kaijage |
KAYA zaidi
ya 86 zilizofukuzwa katika maeneo yao kwa ajili ya kupisha Mgodi wa Madini wa
Geita (GGM) zimeilalamikia serikali kwa kuzitelekeza kaya hizo na kusababisha
watoto kushindwa kwenda shule kupata elimu kama watoto wengine.
Wakitoa malalamiko
yao kwa nyakati tofauti wakazi hao wamedai kuwa tangu mwaka 2007 hadi sasa
wanaishi kama wakimbizi katika nchi yao kutokana na kufukuzwa kwa nguvu ili
kupisha wawekezaji wa mgodi huo.
Wamesema kutokana
na kufukuzwa hivi sasa wanaishi maisha ya taabu kutokana na kutokuwa na shughuli yoyote ya kuwaingizia kipato kama
walivyokuwa wamezoea
Wakizungumza
kwa uchugu wananchi hao wamesema wanasikitishwa na serikali ya CCM ambayo kwa
sasa inatengeneza matabaka makubwa kati ya watu wenye uwezo na wasiokuwa na
uwezo na mbaya zaidi ni ambapo wanawatukuza wawekezaji na kuwadidimiza wazawa
hata kwa kuwapora mali zao.
Aidha wamedai
kuwa kutokana na wananchi hao kuondolewa katika maeneo yao na kutelekezwa
katika mahema mabovu kumesababisha shughuli za kiuchumi kuzorota na wanafunzi
ambao walikuwa wakisoma kushindwa kwenda shule.
Pia walimueleza
mbunge wa Bukombe Prof. Kulikoyela Kahigi(Chadema) kuwa pamoja na mambo mengine
lakini kuishi kwao kwa mahema ambayo ni mabovu kumesababisha baadhi yao
kupatwa na maradhi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupooza viungo vyao na kukosa nguvu.
Wakitoa malalamiko
yao kwa mbunge huyo ambaye alifika katika maeneo ya viwanja vya magereza Mjini
Geita kwa lengo la kujionea adha wanazozipata wakazi hao wamemweleza kuwa mpaka
sasa serikali haitoi msaada wowote na kusababisha maisha yao kuwa magumu zaidi.
“Hapa tulipo
unaweza kuona hakuna hata kitu chochote tuliuza mifugo yetu, mazao yetu pamoja
na akiba ya chakula tuliyokuwa nayo iliharibika kotokana na kuhamishwa kwa nguvu
na kusababisha uharibifu, hata hivyo na wanafunzi kwa sasa hawaendi shule kutokana
na hali ya kiuchumi iliyopo….
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Geita,Alli Kidwaka, alipoulizwa
alisema kuwa tatizo hilo lipo lakini linafanyiwa kazi ili watu hao waweze kulipwa
fidia zao za kupisha Mgodi huo.
No comments:
Post a Comment