Friday, December 7, 2012

UCHAGUZI GHANA LEO

Mwanamke anaeshabikia chama cha NPP akiwa na matumaini ya chama chake kushinda.AFP

Wapiga kura nchini Ghana leo Ijumaa Disemba 07, 2012 wameamkia katika vituo vya kupigia kura kumchagua Rais wa nchi hiyo inayoshikilia rekodi nzuri ya kusimamia vizuri Demokrasia barani Afrika.

Katika Uchaguzi wa leo, wagombea wawili wanachuana kupata nafasi ya kuingia Ikulu,kutoka chama tawala NDC kinachochuana na chama cha Upinzani cha NPP.
 
Nchi ya Ghana iliyoko Magharibi mwa bara la Afrika imefanya uchaguzi mara tano tangu utawala wa kijeshi utamatike mwaka 1992.
   


No comments:

Post a Comment