By Tamim Elyan and Tom Perry
|
Waandamanaji wakiwa nje ya Jengo la Mahakama Kuu Misri.Reuters |
CAIRO |
Sun Dec 2, 2012
Kikundi cha Kiislamu chenye mrengo mmoja na Rais wa Misri Muhamed Mursi kimeilazimisha Mahakama Kuu nchini humo Jumapili ya Desemba 02 kuahirisha shughuli zake kutokana na waandamanaji kuwashinikiza Majaji kutohudhuria shughuli katika koti hiyo ya juu Misri.
|
Askari Polisi wakiwa ndani ya Jengo la Mahakama Kuu kuwazuia Waandamanaji kuingia katika eneo la Mahakama hiyo.Reuters |
Mahakama ya Juu ya Katiba imesema haitaweza kuendelea na shughuli zake wakati Majaji wake wakiwa na Msongo wa mawazo kutokana na shinikizo la waandamanaji.
|
Waandamanaji wakiwa nje ya Jengo la Mahakama hiyo |
Mgogoro wa sasa unafuatia tangazo la Rais Mursi wa nchi hiyo kutangaza Novemba 22 mwaka huu kwamba atajiongezea madaraka na mamlaka ya kuamua baadhi ya mambo, suala ambalo linapingwa vikali na wananchi hususani wafuasi wa chama kilichomweka madarakani cha Udugu wa Kiislamu.
Hata hiyo Majaji wa Mahakama mbalimbali za nchi hiyo pia wamemtaka rais Mursi kufanya mazungumzo na kughaili uamuzi wake wa kujilimbikizia madaraka; hatua ambayo inatafsiriwa na wengi kama Udikteta mpya, huku waandamanaji wakimwita Rais huyo 'Farao mpya' kutokana na hatua yake ya kutaka kujilimbikizia madaraka.
No comments:
Post a Comment