Thursday, November 29, 2012

HALI YA ELIMU YA MSINGI NCHINI BADO INASIKITISHA...

BUKOMBE,
MBUNGE wa Bukombe Mkoani Geita, Profesa Kulikoyela Kahigi (Chadema), amewapiga marufuku viongozi kuwachangisha wananchi michango kwa kisingizio cha kuchangia maendeleo wakati hakuna vikao vya maamuzi vilivyokaa kukubaliana na michango hiyo.
Mmoja wa wanafunzi wa Darasa la Nne akiandika chini jina la shule yake ya Kagwe shule hiyo ina uhaba wa vyumba vya madarasa, nyumba za walimu na vyumba vyote vya mafarasa vina vumbi licha ya kuwa shule hiyo imesajiliwa mwaka 1985.

Kauli hiyo ameitoa wakati akijibu maswali mbalimbali ya wakazi wa kijiji cha Kagwe,kata ya Lyambamigongo walipokuwa wakiuliza na kutaka kujua uhalali wa michango ya kimaendeleo ambayo wananchi uchangishwa na baadaye kupotelea mifukoni mwa baadhi ya viongozi wachache.
Baadhi ya wanafunzi wa darasa la nne wakiwa darasani katika shule ya msingi ya Kagwe kijiji cha Kagwe kata ya Lyambamigongo Wilayani Bukombe Mkoani Geita.

 Aidha mwananchi mwingine ambaye amejitambulisha kwa jina la Sweya Sweya, naye alitaka kujua ni hatua gani ambazo viongozi  ambao uchagisha fedha nyingi kwa madai ya kufanya shughuli za maendeleo lakini hazionekani na kutolea mfano wa jinsi uongozi wa uliopita wa Lyambamigongo ulivyowachangisha wananchi fedha kiasi cha sh.12,000.kila kaya kwa ajili ya ujenzi wa matundu 8 ya choo katika shule ya sekondari bukombe lakini hadi leo hakuna chochote kilichofanyika.
Wanafunzi wa shule ya msingi Kagwe wakiwa darasani wanamsubiria mwalimu aje awafundishe pia majembe yao yanaonekana kwani baada ya masomo ni kilimo.
Picha zote na Danson Kaijage wa HABARI BLOG

No comments:

Post a Comment