- WACHANA MITIHANI ILIYOKUWA IFANYWE JUNI 15
- SHULE YAFUNGWA; WATIMULIWA WAKAWAITE WAZAZI
- ...ZAIDI YA 20 WAWEKWA KIZUIZINI
Na:Baraka Lusajo_Rungwe
Wanafunzi wa Shule hiyo,mapema baada ya fujo(Hisani ya Father Kidevu) |
Wanafunzi hao wamehusika kufanya fujo katika shule hiyo Juni 14,2012 wakidai kutotendewa haki kwa kupikiwa ugali badala ya wali
Akizungumza na HABARIKA Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Masiba Watson amesema Mali zenye thamani ya jumla ya shilingi Milioni 50 zimeharibiwa zikiwemo Kompyuta,Madawati,Madirisha na samani nyingine katika Shule hiyo
Mmoja wa Wanafunzi hao amesema waliamua kugoma kutokana na uongozi wa shule kutengua 'ratiba ya wali' na kuwapikia ugali kwa madai kuwa mchele hautoshi katika hifadhi.
"Mi sielewi bro wazazi wetu ada wanalipa lakini hawa maticha wanazingua hawajatupikia mpunga eti hautoshi" amesema na kuongeza mmoja wa wanafunzi hao (tunaemuhifadhi)
Awali Mkuu wa shule hiyo amesema juhudi za uongozi wa shule kuwataka wanafunzi hao watulie ziligonga mwamba kutokana na ghasia ambazo hazikuweza kutulizwa mapema hadi pale kikosi cha kutuliza ghasia-FFU kilipofika shuleni hapo na kutuliza fujo iliyokuwa ikifanywa na wanafunzi hao
Masiba ameongeza kuwa wanafunzi hao pia wamechana mitihani waliyokuwa waanze kuifanya Juni 15, ambapo karatasi za mitihani hiyo mara baada ya kuchanwa walizisambaza katika viunga vya shule hiyo
Moja ya Jengo lililoharibiwa |
No comments:
Post a Comment