Thursday, June 14, 2012

BAJETI YA SERIKALI MWAKA WA FEDHA 2012/2013: GHARAMA ZA KUPIGA SIMU JUU

Serikali leo (Juni 14,2012) imeongeza gharama ya kodi katika mawasiliano ya simu kutoka tozo la awali asilimia 10% hadi kufikia asilimia 12%.

Simu ya Mkononi

Kufuatia ongezeko hilo la tozo ni itamaanisha kwamba, kuanzia tarehe Mosi mwezi Julai mwaka huu, watumiaji zaidi ya Milioni 20 wa Simu za Mkononi watalazimika kulipa gharama ya ziada kutokana na ongezeko la Kodi

 Akiwasilisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka huu wa fedha 2012/03 Bungeni, Waziri wa Fedha na Uchumi Daktari William Mgimwa amesema ongezeko hilo ni kama ambavyo Tanzania imeridhia mabadiliko ya mfanano na Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC ambayo inalazimisha viwango vya tozo la Mawasiliano viwe na ulinganifu kwa nchi wanachama.

Mara ya Mwisho Serikali iliongeza gharama kwa watumiaji wa Simu katika bajeti ya  mwaka 2007/08 kutoka tozo la asilimia 7% hadi asilimia 10% ambayo sasa imeongezwa hadi kufikia asilimia 12%.

Sekta ya Mawasiliano ya simu ni miongoni mwa sekta nne 4 zinazotajwa kukua kwa kasi nchini ambapo kwa sasa ni sekta inayozalisha mabilioni ya shilingi na kuiingizia serikali mapato kwa kodi inayotozwa kwa simu zinazopigwa ndani na nje ya nchi kwa watumiaji wakubwa na wadogo zaidi ya Milioni 15.

 







No comments:

Post a Comment