Saturday, June 16, 2012

CECAFA:TUNAHITAJI $ 600,000 KWA AJILI YA MAANDALIZI YA MASHINDANO 2012

Nicholas Musonye-Katibu CECAFA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati CECAFA limesema linahitaji kiasi cha Dola za Kimarekani  Laki Sita 600,000 ili kukamilisha maandalizi yenye mafanikio ya Mashindano hayo makubwa katika Ukanda huu yanayotarajia kukipiga kuanzia Julai 14 katika uwanja wa Taifa na Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam

Michuano hiy ambayo ilikuwa ianze Juni 26 ilisogezwa mbele ambapo sasa itaanza tarehe 14 Julai kutokana na kuingiliana na Ratiba za Mechi za Kimataifa zikizihusisha baadhi ya timu ikiwemo Taifa Stars ya Tanzania ambayo inashiriki katika michuano mbalimbali ya kuwania kushiriki katika kombe la dunia

Amavubi Stars

Kwa Mujibu wa Katibu Kiongozi wa CECAFA Nicholas Musonye amesema  michuano hiyo itafanikiwa iwapo kiasi hicho cha fedha kitapatikana kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kukamilisha mashindano hayo

Hata hivyo taarifa iliyotolewa na kuthibitishwa na Shirikisho la Kabumbu Nchini Tanzania TFF zinabainisha kuwa Michuano hiyo itachezwa katika uwanja wa Taifa na Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam ili kupunguza gharama

Michuano hiyo inadhaminiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame kwa kiasi cha Dola za Marekani 60,000 zinazokamilisha zawadi anayopewa mshindi wa michuano hiyo.


No comments:

Post a Comment