Friday, February 3, 2012

MWEKEZAJI ATISHIA 'KUWAMALIZA' WANANCHI MBARALI

Wananchi wanaoishi na kufanya shughuli za kilimo jirani na shamba kubwa la Mpunga katika kijiji cha Kapunga  wilayani Mbarali wameelezea wasiwasi wa kutishiwa kuteketezwa na mwekezaji wa eneo hilo kuwa itakapofikia mwezi wa saba mwaka anaamini kuwa hakuna kiumbe kitakachokuwa kinaishi maenoe hayo

Akizungumza na Ushindi Redio Mwenyekiti wa Kijiji hicho cha kapunga Ramdhani Ali Nyoni amesema kwamba wameshangazwa sana na kauli ya mwekezaji huyo aliyotoa mbele ya Mkuu wa Wilaya hiyo ya  kuwatishia kwamba itakapo fikia mwezi Julai mwaka huu hakuna kiumbe kitakacho kuwa kinaishi maeneo hayo

 Hivyo kutokana na kauli hiyo ya kutishia wazawa wa maeneo hayo Mwenyekiti huyo  ameiomba serikali kumwondoa mwekezaji huyo mapema iwezekanavyo kwani amekuwa akisababisha matatizo yasiyoisha kwa jamii inayoishi kuzunguka shamba hayo

Baadhi ya waanga waliomwagiwa sumu katika mashamba yao amesema kuwa kwa sasa wanasumbuliwa na magonjwa ya ngozi baada ya chache mwekezaji huyo kumwaga sumu katika mashamba yao
Mmoja wa waadhirika wa sakata hilo Katelina SHIPELA amedai kwamba mpaka sasa hana cha kufanya kutokana na kitendo cha mwekezaji huyo kufanya kitendo hicho

Ameongeza kuwa isitoshe yeye ni mjane na analelawatoto yatima pale kwake na mpaka sasa hajui atawalisha nini hao watoto
Akina mama wa Kapunga wakiteka maji
Juhudi za Waandishi wa Habari kumpata Mwekezaji huyo zimegonga mwamba baada ya waandishi kuambiwa kuwa huenda wakapigwa risasi iwapo watamtafuta

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa mbeya Abbas Kandoro alipohojiwa kuhusiana na sakata hilo kwa njia ya simu kutoka Dar es saam amedai kuwa suala hilo amelipata na analitafutia suluhisho

Na kuongeza kuwa wananchi wa Mbarali hususani wajangwa wawe na subira kwani serikali inatambua kilio chao na kuomba uongozi wa kijiji hicho kuonyesha ushirikiano na wananchi wake wakati huu wa tatizo hili

Moja ya Mitambo ya Mwekezaji huyo


Na Bosco Nyambege
03.02.2012

Sehemu ya Shamba la Kapunga

1 comment: