Wednesday, January 25, 2012

MADAKTARI HOSPITALI YA RUFAA NA META JIJINI MBEYA WAGOMA KUTOA HUDUMA

Na: Waandishi Wetu Kamuli Tete na Bosco Nyambege
Wakati mgomo wa Madaktari ukiendelea nchini Madaktari 75 katika Hospitali ya Rufaa Mbeya wamegoma kutoa huduma kuunga Mkono adhmio la Chama cha Madaktari nchini MAT kuwataka Madaktari kote nchini kugoma kwa kutotimiziwa madai yao kwa  muda mrefu
Akizungumza na waandishi wa Habari Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Mbeya Dokta Eliuta Samky amesema kuwa Madaktari waliogoma ni 65 ambao ni wanafunzi INTERNSHIP na 10 ni Madaktari waliosajiliwa.
Ameongeza kuwa, mgomo huo umeathiri utoaji wa huduma za matibabu kwa wagonjwa kwa kiasi kikubwa
Amewashauri wananchi wanaohitaji huduma za matibabu kwenda katika Hospitali binafsi zilizo Karibu na maeneo yao, ili kuepuka athari hasi zinazoweza kujitokeza wakati suala la mgomo huo wa madaktari likiendelea kushughulikiwa na Utawala
Kwa upane wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amesema kuwa suala hilo linaathiri jamii kwa kiasi kikubwa na kuwaomba Maaktari hao kusitisha mgomo huo ili kunusuru afya za wananchi wakati madai yao yakishughulikiwa na serikali.
Nao Madaktari walipotakiwa kuzungumza lolote kuhusiana na mgomo huo hawakuwa tayari na badala yake wakatoa waraka unaobainisha madai yao ambapo miongoni mwa madai ni Kuboreshwa kwa huduma za afya kwa wagonjwa,maslahi duni kwa watumishi wa sekta ya afya,malipo ya muda wa ziada wa kazi,madai ya kupewa nyumba au fedha ya kupanga nyumba,posho ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi,na Madai ya kumtaka Katibu Mkuu Wizara ya Afya Blandina Nyoni kujiuzulu.
Katika waraka huo pia Madaktari hao wameazmia kuendelea na Mgomo usio na kikomo kuanzia Jumanne tarehe 24 Januari,2012 hadi madai yao yatakapopatiwa ufumbuzi,kuendelea na vikao vya ndani kwa wafanazyakazi wa sekta ya Afya,na Mengineyo yatakayojiri.




No comments:

Post a Comment