Wednesday, October 19, 2011

JESHI LA POLISI MKOANI DODOMA LAWASWEKA NDANI VIONGOZI WA CHADEMA KWA KUKIUKA AGIZO...


JESHI la polisi Mkoa wa Dodoma limewashweka ndani viongozi 11 wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa madai kuwa wamekiuka maelekezo ya jeshi hilo la kuwazuia kufanya mkutano wa hadhara.

Baadhi ya viongozi waliokamatwa na jeshi hilo ni pamoja na Mkurugenzi wa Oganaizeisheni na Mafunzo katika chama hicho taifa, Benson Kigaira, katibu wa mkoa wa Dodoma Stiven Masawe, katibu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Jera Mambo.

Wengine waliokamatwa na jeshi hilo ni pamoja na Mjumbe wa baraza kuu Taifa Alex Necrous, katibu wa wazee wilaya ya Dodoma mjini Ahamed Sango, Magrethi Thadei ambaye ni katibu wa wanawake Wilaya ya Dodoma Mjini pamoja na Alidi Zoya ambaye ni mwanachama wa chama hicho.

Pia katika viongozi waliokamatwa ni pamoja na Enock Mhembano ambaye alikuwa ngombea ubunge jimbo la Dodoma mwaka jana, Yusufu Kunti ambaye ni katibu wa baraza la wanawake mkoa wa Dodoma na dereva kutoka makao makuu Juma waziri.

Aidha zimetajwa mali nyingine ambazo zimechukuliwa na jeshi la polisi ni pamoja na bendera za chama hicho, Viti ikiwa ni pamoja na kuwatawanya wananchi ambao tayari walishakusanyika kwa ajili ya kusikiliza mkutano huo ambao ulitakiwa ufanyike katika uwanja wa barafu mjini hapa.

Kwa mujibu wa katibu wa Vijana mkoa wa Dodoma Idd Kizota, alisema kuwa kitendo kilichofanywa na jeshi la polisi ni cha kihuni kwani chama hicho kiliandika barua ya kuomba kibari tangu 16 Ocktoba mwaka huu.

Kizota alisema kuwa barua iliyoandikwa na chama hicho kwa ajili ya kuomba kibari cha mkutano ilikuwa na kumbukumbu namba CDM/WLY/OCD/TM/VOL.11/ ya tarehe 16.10.2011 ambapo walipewa majibu ya kufanya mkutano huo.

Kiongozi huyo pia alisema kuwa pamoja na kuwazuia viongozi hao na kuwakamata ni kuingilia uhuru wa sheria za vyama kwani barua ya zuio iliandikwa saa 5 na dakika 20 jambo ambalo ni kinyume na utoaji wa zuia katika mikutano ya hadhara.

Hata hivyo alisema kuwa jeshi la polisi halikuwa na sababu yote ya kuzuia mkutano bali walitakiwa kuongeza nguvu ya ulinzi ili kuwapa fursa ya kufanya mkutano ambao lengo lake kubwa ni kuhakikisha wanatoa elimu ya uraia kwa wananchi.

Kwa upande wa Ofisa wa Jeshi la polisi ambaye akutaka kutajwa jina lake kwa madai kuwa siyo msemaji alithibitisha kukamatwa kwa viongozi hao kwa madai kuwa wamekaidi amri halala ya kutofanya mkutano na kujaribu kufanya mkutano huo.

Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Zeloth Stivine hakuweza kuonyesha ushirikiano juu ya tukio hilo kwa maana alikuwa akipigiwa simu bila kupokelewa

No comments:

Post a Comment