BARAZA la wafanyakazi la Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi limeunda kamati ya kikosi kazi kwa ajili ya kufuatilia madeni mbalimbali ya watumishi nchini katika Wizara hiyo.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa baraza la Wafanya kazi Serestine Gesimba, ambaye pia ni Naibu katibu mkuu wa Wizara ya hiyo wakati wa kufunga mkutano wa 20 wa baraza la wafanyakazi la Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi uliofanyika mjini hapa.
Gesimba alisema kuwa kikosi kazi hicho kimeundwa kutokana na maazimio ya mkutano huo wa baraza la wafanyakazi kwa lengo la kuhakikisha kikosi kazi hicho kitafuatilia mambo malimbali ikiwa ni pamoja kufuatilia matatizo yanayowakumba walimu.
Akiongelea kuhusu kuundwa kwa kamati ya kikosi kazi hicho alisema kuwa kitafanya kazi kubwa ya kufuatilia changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo walimu kwa kucheleweshewa miashara yao pamoja na kutopandishwa nadaraja.
Aidha alisema kuwa pamoja na kuundwa kwa kamati ya kikosi kazi pia wameunda kamati ya utendaji, kwa ajili ya kupitia changamoto mbalimbali ambazo zitapelekwa katika mkutano mkuu wa wafanya kazi katika mkutano mkuu wa baraza hilo mwaka kesho.
Gesimba pia aliitaka Wizara ya Elimu kuhakikisha inaharakisha kulipa madeni mbayo yamekuwa yakidaiwa na watumishi ili kuweza kukuza utendaji wa kazi badala ya kuwakatisha watumishi.
Akiongelea juu ya maazimio yaliyotolewa na baraza hilo pia aligusia mikakati iliyowekwa na baraza hilo ili kuweza kutoa elimu kwa jamii ili waweze kutambua mipaka na kazi ziazofanywa na TAMISEMI na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Alisema kuwa bado jamii aina uelewa wa kutosha hivyo wanashindwa kutenganisha majukumu ya kazi zinazofanywa na TAMISEMI na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi jambo ambalo linasababisha kuwepo kwa mtafaruku kati ya watumishi na Wizara husika.
Akifunga mkutano 20 wa baraza hilo , Katibu Tawala mkoani hapa, Rehema Madenge aliwataka wajumbe wa kuhakikisha wanafanya kazi zenye tija kwa ajili ya mafanikio kwa taifa.
Aliwataka kuepukana na migogoro katika sehemu za kazi na badala yake wawe wasimamizi wa amani na ushauri ndani ya vituo vyao vya kazi.
Aidha aliwashawishi kutembelea Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa madai kuwa ni sehemu ya utalili katika mkoa wa Dodoma .
Madenge, aliipongeza wizara kwa kuunda baraza la wafanyakazi kwa ajili ya kutoa msukumo kwa wadau wote wa elimu ili kuweza kuboresha huduma kwa uuma.
“Huu ndiyo uongozi bora unaotakiwa kuimarishwa mahala pa kazi,” alisema
No comments:
Post a Comment