Wednesday, October 19, 2011

MKAZI MMOJA JIJINI HAPA JUMATANO HII KAPANDA KIZIMBANI KUJIBU MASHTAKA YA KUKUTIKANA NA KARATASI ZA KUFYATULIA NOTI ZISIZO HALALI KWA MALIPO YA TSH

19/10/2011

MAHAKAMA ya hakimu mkazi jijini Mbeya Jumatano hii imesikiliza kesi inayomkabili JOSEPH MICHAEL MAWENZI(30) kwa makosa mawili tofauti aliyoyafanya kati ya April 14 mwaka 2010 na may 3 mwaka huu likiwemo kosa la kukutwa na karatasi za kutengeneza noti bandia.

Akisoma shauri la kwanza wakili wa serikali ROJAZ MASAWE mbele ya hakimu mkazi ZABIBU MPANGULE amesema, mnamo mwezi May 3 mwaka huu, mshtakiwa alipatikana na makaratasi ya kutengenezea noti bandia pamoja na frame na wino vifaa ambavyo vimeelezwa hutumika kufyatulia noti bandia, kinyume na kifungu cha sheria namba 341 “a” sura ya 16 kama kilivyo fanyiwa marekebisho mwaka 2002.

katika kosa la pili mshitakiwa amesomewa shitaka lake na wakili ACHILIS MULISA mbele ya hakimu mkazi KUSAGA MAJINGE ambapo amesema mnamo April 4,2010 maeneo ya SOWETO mshitakiwa alijipatia pesa kwa njia ya utapeli sh.laki 3 na nusu kutoka kwa MUSHI NDESAMULO ambapo ni kinyume na kifungu cha sheria namba 302 sura ya 16 kama kilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Mshitakiwa amekana makosa yote mawili na ametakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao ni wafanyakazi serikalini ambao watamdhamini kwa sh. Million 1 kila mdhamini.

Mshitakiwa ameshindwa kutimiza masharti aliyopewa na mahakama imeamuru arudishwe rumande hadi tarehe 2 Novemba kesi yake itakaposikilizwa tena

No comments:

Post a Comment