Na.Tamimu Adamu, Jeshi la Polisi
JESHI Polisi Mkoani Mtwara limefanikiwa kukamata gari lenye namba za usajili T.867 aina ya Toyota Carina Saloon likiwa limebeba shehena ya mifuko yenye meno ya Tembo tisini (90) yenye uzito wa kilogramu 222.1 ya thamani zaidi ya shilingi bilioni moja (1,082, 025,000/=)/
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Zelothe Steven alisema kuwa gari lilikamatwa kata ya Maendeleo, wilaya ya Masasi katika barabara kuu ya
Tunduru kuelekea Masasi.
Zelothe alisema kuwa askari wa doria walilitilia shaka gari hilo na kumuamuru dereva kusimama kuonyesha leseni ya udereva ambapo dereva wa gari hilo hakuwa nayo, ndipo askari alichukua hatua ya kufanya ukaguzi ambapo alikuta gari hilo limejaza shehena ya mifuko inayosadikiwa kuwa ni meno ya Tembo.
“Askari waliamua kulifisha gari hilo kwenye kituo kikuu cha Polisi wilaya ya Masasi umbali wa kilometa moja kutoka sehemu lilipokamatwa gari hilo, wakati wakiwa njiani kuelekea kituoni dereva na mwenzake walikuwa wakimshawishi askari huyo waelewane ili wampatie shilingi milioni tatu aweze kuwaachia lakini askari huyo alikataa na kufanikiwa kulifikisha gari hiyo kituoni” Alisema Zelothe.
Alisema kuwa kabla gari hilo halijasimama vizuri dereva na mwenzake waliruka na kutokomea vichochoroni, juhudi za kuwasaka bado zinaendeleaili waweze kukamatwa na kufikishwa mahakamani*.*
Miongoni mwa vitu vilivyokutwa ndani ya gari hilo wakati wa upekuzi nipamoja na simu moja ya kiganjani aina ya Techno, mizani aina ya tonash,fomu za “notification” pamoja na Bank slip.
Kutokana na uchunguzi uliofanyika imebainika kuwa dereva wa gari hiloanatajwa kuwa ni Oliver Lucas mkazi wa Masasi na mwenzake aliyekuwa nayebado hajatambulika na inaaminika kuwa tajili wao ni mtu mwenye jina laHassan Koko anayejulikana kwa jina maarufu la Twalib Nyoni.
Kamanda Zelothe amewataka wananchikuongeza kasi ya kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili kuweza kukomesha biashara hii haramu ya usafirishaji wa nyara za Serikalina kutoa taarifa zitakazowezesha kukamatwa kwa watuhumiwa hao ili waweze kufikishwa katika vyombo vya
sheria.
No comments:
Post a Comment