Sunday, February 3, 2013

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MBEYA




Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani

Wilaya ya mbeya mjini - mauaji



Mnamo tarehe 03.02.2013 majira ya saa 18:00hrs huko katika hospitali ya rufaa mbeya. Ambokile s/o kikwale,miaka 16,mnyiha,mkulima mkazi wa ilemi alifariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo baada ya kupigwa kwa kutumia fimbo ngumi na mateke na mama yake mdogo [mama wa kambo ]  bupe w/o joseph kikwale,kyusa,miaka 32,mkulima mkazi wa ilemi  majira ya saa 17:00hrs .chanzo ni mtuhumiwa kumtuhumu marehemu kuwa anamuibia pesa nyumbani kwake  eneo la isanga. Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitalini hapo. Mtuhumiwa amekamatwa na taratibu za kumfikisha mahakamani zinafanywa. Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi wa polisi diwani athumani anatoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na badala yake watatue matatizo ya kifamilia kwa njia ya mazungumzo ili kuepusha matatizo yanayoweza kuepukika.





Wilaya ya rungwe - ajali ya gari na kusababisha kifo



Mnamo tarehe 02.02.2013 majira ya saa 19:00hrs huko katika kijiji cha lwangwa wilaya ya rungwe mkoa wa mbeya. Ipyana s/o silwimi,miaka 36,kyusa ,dereva mkazi wa kijiji cha kikota aliruka kutoka kwenye gari t.482 ayb aina ya isuzu alilokuwa akiendesha kisha gari hilo kumkanyaga . Marehemu alifariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa katika hospitali ya misheni itete kwa matibabu. Chanzo cha ajali ni gari kushindwa kupanda mlima na kurudi nyuma ambapo dereva aliamua kuruka  na gari kumkanyaga. Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi wa polisi diwani athumani anaendelea kutoa wito kwa madereva kuwa makini kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuwa na tahadhari wanapotumia vyombo vya moto ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.





Wilaya ya chunya - kupatikana na bhangi.



Mnao tarehe 03.02.2013 majira ya saa 11:30hrs huko katika kijiji cha mbangala wilaya ya chunya mkoa wa mbeya. Askari polisi wakiwa doria walimkamata frenk s/o hamisi,miaka 25,mkulima,mnyiha,mkazi wa kijiji cha chang’ombe akiwa na bhangi kete 44 sawa na gram 220  . Mtuhumiwa ni muuzaji na mvutaji wa bhangi.taratibu za kisheria zinafanywa ili mtuhumiwa faikishwe mahakamani. Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi wa polisi diwani athumani anaendelea kutoa wito kwa jamii kuacha kutumia dawa za kulevya kwani ni kinyume cha sheria na ni hatari kwa afya ya mtumiaji.

 





Signed by,

[diwani athumani – acp]

Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya.

No comments:

Post a Comment