Tuesday, January 22, 2013

Makamu wa Rais Dkt. Bilal ahudhuria maziko ya Makamu wa Rais wa Zimbabwe jijini Harare

_DSC0249 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akifurahia jambo na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe kwenye Ikulu ya nchi hiyo jijini Harare  baada ya kumaliza  mazungumzo yao.  Makamu wa Rais alimtembelea Rais Mugabe kwa lengo la  kumfariji kutokana na kifo cha Makamu wake Marehemu Dkt. Landa John Nkomo kilichotokea mwanzoni mwa wiki iliyopita.  Dkt. Nkomo   alizikwa jana kwenye Makaburi ya Mashujaa jijini Harare .
PICHA NA OMR
_DSC0240 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal kushoto akizungumza na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe alipomtembelea  Ikulu ya Harare  jana  kwa lengo la  kumfariji kutokana na kifo cha Makamu wa Rais wa nchi hiyo Marehemu  Dkt.  Landa John Nkoma kilichotokea mwanzoni mwa wiki iliyopita na kuzikwa jana katika Makaburi ya Mashujaa jijini Harare. Katikati  ni Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe  Adadi Rajabu.
_DSC0220 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka shada la maua kwenye kaburi la Makamu wa Rais wa Zimbabwe Marehemu Dkt. Landa John Nkomo wakati wa mazishi yake yaliyofanyika jana  kwenye Makaburi ya Mashujaa jijini Harare.
_DSC0190 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mkewe Mama Asha Bilal, wakiwa katika Viwanja vya Makaburi ya Mashujaa jijini Harare,  walipohudhuria maziko ya Makamu wa Rais wa Zimbabwe Marehemu Dkt. Landa John Nkomo  yaliyofanyika jana  jijini Harare Zimbwabwe.

No comments:

Post a Comment