Wagonjwa na ndugu wa wagonjwa waliolazwa katika wodi hilo
wakishuhudia tukio hilo baada ya hakimu mkazi ,mwandamizi mfawidhi
wa mahakama ya mkoa wa Iringa Juma Hasan kumaliza kushughuli za
kimahakama Hospitalini hapo
DEREVA
wa basi la Msanya Trans ambalo lilitapa ajali mbaya jumamosi ya wiki
iliyopita na kusababisha vifo vya watu 11 na kujeruhi wengine zaidi
ya 20 katika eneo la Kichakani kwenye barabara kuu ya Iringa -Mbeya
amesomewa mashitaka 40 akiwa wodi
ni katika Hospitali ya mkoa wa Iringa.
ni katika Hospitali ya mkoa wa Iringa.
Wakisoma
mashtaka hayo leo katika wodi namba 5 Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa
Iringa ,mbele ya hakimu mkazi ,mwandamizi mfawidhi wa mkoa wa Iringa
Juma Hassan wakili wa serikali Adolph Maganda akisaidiwa na msaidizi
wake Hamad Magenda alisema kuwa mtuhumiwa huyo katika kesi hiyo
namba 90 ya mwaka 2012 ya usalama barabarani anatuhumiwa kutenda makosa
hayo Desemba 8 mwaka huu .
Alisema kuwa mtuhumiwa huyo Bw Rashid Selemani Msanya (35)
ambae alikuwa ni dereva wa basi hilo la Msanya Trans lenye namba za
usajili T 803 AJV Nissan ambalo lilikuwa likitokea Iringa mjini kwenda
Usokami wilaya ya Mufindi alisababisha ajali na kupelekea vifo vya
watu 11 waliokufa katika ajali hiyo.
Wakili
Magande alisema kuwa mtuhumiwa huyo anatuhumiwa kwa makosa 40 ambapo
jumla ya makosa 11 ni ya kusababisha vifo na makosa 28 ni ya
kusababisha majeruhi na kosa moja kati ya 40 ni kusababisha ajali na
kuharibu gari hilo.
Hata
hivyo mtuhumiwa huyo amekana makosa yote na kuendelea kuwa chini ya
ulinzi wa polisi wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika
Hospitali hiyo ya mkoa wa Iringa akitibiwa majeraha makubwa ya moto
ambao unasadikika kutokana na maji ya rejeta ya basi hilo.
Hakimu
wa mahakama hiyo mheshimiwa Hassan alimnyima dhamana mtuhumiwa huyo
hadi kesi hiyo itakapotajwa tena Desemba 20 mwaka huu na kuwa mtuhumiwa
ataendelea kuwa chini ya ulinzi wa polisi katika Hospitali hiyo.
No comments:
Post a Comment