Wanamichezo
50 kati ya 52 waliochukua fomu kuomba kuwania nafasi mbalimbali za
uongozi katika uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
utakaofanyika Februari 24 mwaka huu wamerejesha fomu hizo.
Waombaji
ambao hawakurejesha fomu ni Geofrey Nyange aliyekuwa akiomba ujumbe wa
Kamati ya Utendaji kuwakilisha mikoa ya Morogoro na Pwani, na Shufaa
Jumanne aliyekuwa akiomba kuwakilisha Kanda ya Dar es Salaam.
Orodha
kamili ya waombaji ambao wamerejesha fomu ni Athuman Nyamlani, Jamal
Malinzi, Omari Nkwarulo na Richard Rukambura (Rais). Michael Wambura,
Ramadhan Nassib na Wallace Karia (Makamu wa Rais).
Kwa
upande wa ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Abdallah Musa, Salum Chama na
Kaliro Samson (Kagera na Geita), Jumbe Magati, Mugisha Galibona,
Richard Rukambura, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara
na Mwanza).
Epaphra
Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo, Elly
Mbise na Omari Walii (Arusha na Manyara), Ahmed Mgoyi na Yusuph Kitumbo
(Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Blassy Kiondo, Nazarius Kilungeja
na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James Mhagama na Stanley Lugenge
(Njombe na Ruvuma).
Athuman
Kambi, Francis Ndulane na Zafarani Damoder (Lindi na Mtwara), Hussein
Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na Singida), Farid Nahdi, Hassan Othman
Hassanoo, Riziki Majala na Twahili Njoki (Morogoro na Pwani), David
Lugenge, Elias Mwanjala, Eliud Mvella na John Kiteve (Iringa na Mbeya),
Davis Mosha, Khalid Mohamed na Kusiaga Kiata (Kilimanjaro na Tanga) na
Alex Kamuzelya, Juma Pinto, Muhsin Balhabou, Omari Abdulkadir na Shaffih
Dauda (Dar es Salaam).
6 WAOMBA UONGOZI BODI YA LIGI KUU, WOTE WAREJESHA FOMU
Waombaji
wote sita wa uongozi katika Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) ambayo
uchaguzi wake utafanyika Februari 22 mwaka huu wamerejesha fomu.
Kwa
upande wa Mwenyekiti waombaji ni Hamad Yahya wa Kagera Sugar na Yusuph
Manji wa Yanga wakati Makamu Mwenyekiti aliyeomba ni Said Mohamed wa
Azam.
Nafasi
mbili za ujumbe wa Bodi ya Ligi Kuu kwa klabu za Daraja la Kwanza
zimeombwa na watu watatu. Waombaji hao ni Christopher Peter Lunkonde wa
Moro United, Kazimoto Miraji Muzo wa Pamba ya Mwanza na Omari Khatibu
Mwindadi.
Kamati
ya Uchaguzi ya TFF itaanza kukutana kesho kwa ajili ya kupitia fomu
zote zilizowasilishwa na waombaji kwa ajili ya uchaguzi wa TFF na ule wa
Bodi ya Ligi Kuu.
Pia
Kamati inapenda kuwakumbusha waombaji uongozi kuzingatia Kanuni za
Uchaguzi, kwani baadhi yao wameanza kufanya kampeni kupitia vyombo vya
habari. Kwa walioanza kufanya kampeni kabla ya wakati wanajiweka katika
hatari ya kuenguliwa kushiriki katika uchaguzi.
No comments:
Post a Comment